KOCHA Kenny Dalglish atamuwakilisha Luis Suarez katika upokeaji wa tuzo ya Kiatu cha Dhahabu Jumatano ijayo mjini Barcelona kufuatia ombi maalum la mshambuliaji huyo wa Uruguay.
Suarez alisajiliwa Liverpool wakati Dalgish akiwa kocha mwaka 2011 na wawili hao wataungana tena wiki ijayo wakati mshambuliaji huyo anachukua tuzo ya mabao yake 31 msimu uliopita.
Mshambuliaji huyo wa Barcelona alitaka Mscotland huyo na Nahodha wake wa zamani, Steven Gerrard wahudhurie hafla hiyo– lakini Nahodha wa Liverpool hataweza kufika, ila kocha wake wa zamani atasafiri kwenda Hispania Jumatano kwenye shughuli hiyo.
Dalglish alimkingia sana kifua Suarez wakati wapo naye Liverpool hususan wakati ambao alikuwa anakabiliwa na tuhuma za kumfanyia vitendo vya kibaguzi Patrice Evra.
Suarez pia anataka afanye sherehe fulani Anfield lakini adhabu yake ikiwa imebakiza siku 15 inaweza kumzuia kufanya hivyo kwa sasa. Mechi ijayo ya Liverpool itakuwa dhidi ya Hull Oktoba 25, lakini nyota wao huyo wa zamani ndiyo atakuwa anacheza mechi yake ya kwanza ya mashindano tangu asajiliwe Barcelona, wakimenyana na wapinzani wao, Real Madrid katika El Clasico Uwanja wa Bernabeu. Lionel Messi, mchezaji mwenzake Suarez ndani ya Barcelona alishinda Kiatu cha Dhahabu misimu miwili iliyopita.

![]() |
Kenny Dalglish kulia akiwa na Luis Suarez enzi zao Liverpool |
Dalglish alimkingia sana kifua Suarez wakati wapo naye Liverpool hususan wakati ambao alikuwa anakabiliwa na tuhuma za kumfanyia vitendo vya kibaguzi Patrice Evra.
Suarez pia anataka afanye sherehe fulani Anfield lakini adhabu yake ikiwa imebakiza siku 15 inaweza kumzuia kufanya hivyo kwa sasa. Mechi ijayo ya Liverpool itakuwa dhidi ya Hull Oktoba 25, lakini nyota wao huyo wa zamani ndiyo atakuwa anacheza mechi yake ya kwanza ya mashindano tangu asajiliwe Barcelona, wakimenyana na wapinzani wao, Real Madrid katika El Clasico Uwanja wa Bernabeu. Lionel Messi, mchezaji mwenzake Suarez ndani ya Barcelona alishinda Kiatu cha Dhahabu misimu miwili iliyopita.
0 comments:
Post a Comment