SIMBA SC inatarajiwa kuondoka leo kwenda Afrika Kusini kwa maandalizi ya mchezo dhidi ya watani wa jadi, Yanga SC Oktoba 18, mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Simba SC itakuwa huko hadi Oktoba 17, itakaporejea nchini kwa ajili ya mchezo huo na mahasimu wao wa kihistoria, Yanga SC.
Ni mchezo wa kawaida wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara- ambao timu zitawania pointi tatu za kujiweka vizuri kwenye msimamo.
Simba SC haijashinda mechi hata moja kati ya tatu ilizocheza, ikitoa sare zote, 2-2 na Coastal Union, 1-1 na Polisi Morogoro na 1-1 na Stand United.
Mahasimu wao, Yanga SC wamevuna pointi sita katika mechi tatu, wakishinda mbili dhidi ya Prisons na JKT Ruvu, 2-1 kila mechi na kufungwa moja, 2-0 na Mtibwa Sugar.
Simba SC imeuanza msimu ikiwa na safu mpya ya uongozi, chini ya Rais Evans Elieza Aveva na Makamu wake, Geoffrey Nyange ‘Kaburu’ kufuatia uchaguzi wa Mei 29, mwaka huu.
Wapenzi, wanachama na mashabiki wa Simba SC waliupokea kwa furaha uongozi mpya, wakiamini huo ni mwanzo wa zama mpya katika klabu yao, za kufurahia ndani na nje ya Uwanja.
Sera za pointi tatu za Aveva wakati anaomba kura, ziliongeza matumaini kwa wana Simba SC na kwa kufahamu ni mfuasi wa kundi la Friends Of Simba (F.O.S.) linaloundwa na watu walio njema kiuchumi, imani ilikuwa kubwa sana.
Hivyo matokeo ya sare tatu mfululizo, kidogo yamewarudisha nyuma wana Simba SC na kuanza kukata tamaa, kwamba huenda wametoa uongozi ‘afadhali’ na kuingiza uongozi ‘bure’.
Kocha Patrick Phiri aliwasili nchini Agosti 13, mwaka huu kuchukua nafasi ya Zdravko Logarusic aliyefukuzwa baada ya timu kufungwa 3-0 na ZESCO United ya Zambia katika tamasha la Simba Day.
Maana yake alianza kuiandaa timu rasmi siku mbili baadaye na Ligi Kuu ilianza Septemba 20- yaani Phiri, raia wa Zambia alikuwa ana mwezi mmoja tu wa kuiandaa timu ambayo hakuisajili yeye kabla ya kuingia kwenye ligi.
Bahati mbaya zaidi, baa la majeruhi nalo likachukua nafasi yake na katika kipindi cha wiki tatu za ligi, Phiri amekwishawakosa Ivo Mapunda, Paul Kiongera, Jonas Mkude, Miraj Adam, Nassor Masoud ‘Chollo’, Issa Rashid ‘Baba Ubaya’ na Haroun Chanongo.
Wachezaji hao ndiyo walioifanya Simba SC chini ya Phiri ing’are katika michezo yake ya kirafiki- lakini kuanza Ligi Kuu mambo yakabadilika.
Inawezekana kuna makosa yalifanyika katika usajili, wakaachwa wachezaji wasiostahili kuachwa ili kutoa nafasi ya kuingiza wachezaji wapya. Inawezekana.
Lakini kitu ambacho wana Simba SC wanatakiwa kuelewa ni kwamba, wapo katika kipindi kigumu cha mpito, chini ya uongozi mpya na kocha mpya.
Nani ana wasiwasi juu ya uwezo wa Phiri? Huyo ni kati ya walimu bora Afrika wenye rekodi za mafanikio.
Yupo mwenye wasiwasi na uongozi wa klabu chini ya Rais Aveva? Aveva ni kiongozi mzuri, mwenye mapenzi ya dhati na Simba SC- ambaye ana uzoefu na siasa za soka ya Tanzania.
Na vizuri zaidi, nyuma yake wapo F.O.S. ambao ni magwiji wa fitina na siasa za soka ya nchi hii- ambao sina shaka watairudisha timu kwenye mstari.
Lakini hilo si jambo la kutarajia mapema sana, kwa sababu wanahitaji kwanza kujipanga na kujiweka sawa, kwa kuanzia kuwa na timu bora na wao pia kama viongozi kuweka mipango yao sawa.
Mara nyingi huwa ninaandika, kusajili wachezaji wazuri ni jambo moja- lakini ili kuwa na timu nzuri yanahitajika maandalizi.
Hadi sasa, naona Simba SC wanakwenda vizuri katika maandalizi, timu inakuwa kambini muda mrefu, hakuna malalamiko kuhusu maslahi ya wachezaji na hata wachezaji wanaoumia, wanatibiwa vizuri.
Jambo ninaloweza kuwaambia wana Simba SC, wawe na subira. Waupe muda uongozi wao ufanye kazi ili kuirudisha timu kwenye mstari.

0 comments:
Post a Comment