Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
MPASUKO mkubwa unainyemelea soka ya Tanzania kufuatia taarifa za kuwapo uhasama mzito baina ya Rais wa Shirikisho la Soka (TFF), Jamal Malinzi na kigogo wa kundi la Friends Of Simba, Kassim Mohamed Dewji.
Mpasuko huo unavuka mipaka kutoka kuwa wa wawili hao- hadi kuwa wa taasisi, yaani Simba SC kwa ujumla na TFF, kila mmoja baina yao akitumia chombo chake katika mapambano.
Tayari kuna imani ya Simba SC kuchukiwa na TFF ya Malinzi- na kadhalika TFF wanaamini wanapigwa vita na Friends Of Simba (F.O.S).
Mara baada ya timu ya taifa, Taifa Stars kutolewa na Msumbiji katika mechi ya kuwania kupangwa kwenye makundi ya kuwania tiketi ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) mwakani, kambi ya Malinzi ilivujisha habari kwamba timu hiyo ilihujumiwa na vigogo wa klabu kubwa.
Na siku chache baadaye, Malinzi akasema ataunda Kamati ya kuchunguza tuhuma hizo, vigogo mbalimbali wakiitwa kuhojiwa na akaomba watoe ushirikiano, huku akiweka mkwara ambaye hatatoa ushirikiano atachukuliwa hatua.
Wakati bado matokeo ya tuhuma hizo hayajatoka- Simba SC nao wanadai wana ushahidi wa kutosha, Malinzi amekuwa ‘akitia mkono’ kwenye mechi zao za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
Simba SC imecheza mechi tatu mfululizo za Ligi Kuu bila kushinda, ikitoa sare zote, 2-2 na Coastal Union na 1-1 mara mbili mfululizo na Polisi Moro na Stand United, tena mechi zote ikicheza Uwanja wa nyumbani, Taifa, Dar es Salaam.
Baada ya sare ya Jumamosi na Stand, Friends Of Simba wakaibua tuhuma kwamba Msaidizi wa Malinzi, Juma Matandika alikuwa na marefa wa mchezo huo siku moja kabla ya mechi.
Na tuhuma hizi zinakuja wakati ambao kuna mgogoro mzito baina ya Bodi ya Ligi na Kamati ya Utendaji ya TFF juu ya makato ya asilimia tano kutoka fungu la fedha la udhamini wa ligi hiyo kuingia kwenye mfuko wa Maendeleo ya Vijana.
Serikali, kupitia Wizara inayohusika na michezo imeupoza mgogoro huo kwa kuiagiza TFF ikutane na Klabu za Ligi Kuu kuwasilisha ombi hilo badala ya kutaka kulazimisha kukata asilimia tano, tu kwa mawasiliano yake na uongozi wa Bodi ya Ligi.
NINI CHANZO CHA UHASAMA WA MALINZI NA DEWJI?
Kassim Dewji maarufu kwa jina la utani KD, kwa muda mrefu amekuwa na tenda ya kuwauzia TFF jezi za timu za taifa, lakini tenda hiyo ilikatika baada ya Malinzi kuingia ofisini Oktoba mwaka jana.
Inadaiwa kabla ya tenda hiyo kukatika, Malinzi aliwahi kuwa na kikao na Dewji ambacho mwisho wake ni matokeo ya tenda hiyo kufa. Inadaiwa, tangu hapo wawili hao wamekuwa na uhasama wa chinichini hadi sasa unaelekea kuwa wazi.
Inadaiwa sababu kubwa ya Malinzi kuonekana anataka kumbeba Michael Wambura katika uchaguzi wa Simba SC ni kwa kuhofia F.O.S. wakiingia madarakani kwenye klabu hiyo atakuwa na wakati mgumu TFF.
Na uhusiano wa Malinzi na Friends of Simba ulianza kuingia doa wakati huo wa uchaguzi wa Simba SC- kwani F.O.S. waliona Rais huyo wa TFF anawasaliti baada ya kumsaidia kwa hali na mali wakati wa uchaguzi wa shirikisho.
F.O.S. wanadai wao ndio waliombeba Malinzi katika uchaguzi wa TFF baada ya aliyekuwa mpinzani wake mkubwa, Athumani Nyamlani kuwa anasaidiwa na mahasimu wa Simba SC, Yanga SC.
Malinzi na Dewji wote hawakupatikana kuzungumzia tuhuma hizo- ingawa BIN ZUBEIRY inaendelea na jitihada za kuwatafuta kwa ajili ya kuelezea hilo.
Dewji alipokea simu mara moja wiki iliyopita na kusema yuko kwenye kikao apigiwe baadaye, lakini baada ya hapo akawa hapokei simu. Malinzi alikwepa kuzungumzia hayo wiki iliyopita akidai ana haraka na tangu hapo amekuwa hapokei simu pia.

![]() |
Vita hatari; Rais wa TFF, Jamal Malinzi kushoto na kigogo wa F.O.S., Kassim Dewji wanadaiwa kuhitilafiana |

Jezi za Uhlsport ambazo Kassim Dewji alikuwa akiwauzia TFF |
NINI CHANZO CHA UHASAMA WA MALINZI NA DEWJI?
Kassim Dewji maarufu kwa jina la utani KD, kwa muda mrefu amekuwa na tenda ya kuwauzia TFF jezi za timu za taifa, lakini tenda hiyo ilikatika baada ya Malinzi kuingia ofisini Oktoba mwaka jana.
Inadaiwa kabla ya tenda hiyo kukatika, Malinzi aliwahi kuwa na kikao na Dewji ambacho mwisho wake ni matokeo ya tenda hiyo kufa. Inadaiwa, tangu hapo wawili hao wamekuwa na uhasama wa chinichini hadi sasa unaelekea kuwa wazi.
Inadaiwa sababu kubwa ya Malinzi kuonekana anataka kumbeba Michael Wambura katika uchaguzi wa Simba SC ni kwa kuhofia F.O.S. wakiingia madarakani kwenye klabu hiyo atakuwa na wakati mgumu TFF.
Na uhusiano wa Malinzi na Friends of Simba ulianza kuingia doa wakati huo wa uchaguzi wa Simba SC- kwani F.O.S. waliona Rais huyo wa TFF anawasaliti baada ya kumsaidia kwa hali na mali wakati wa uchaguzi wa shirikisho.
F.O.S. wanadai wao ndio waliombeba Malinzi katika uchaguzi wa TFF baada ya aliyekuwa mpinzani wake mkubwa, Athumani Nyamlani kuwa anasaidiwa na mahasimu wa Simba SC, Yanga SC.
![]() |
Jezi za sasa za Taifa Stars baada ya Malinzi kumkatia tenda Dewji |
Malinzi na Dewji wote hawakupatikana kuzungumzia tuhuma hizo- ingawa BIN ZUBEIRY inaendelea na jitihada za kuwatafuta kwa ajili ya kuelezea hilo.
Dewji alipokea simu mara moja wiki iliyopita na kusema yuko kwenye kikao apigiwe baadaye, lakini baada ya hapo akawa hapokei simu. Malinzi alikwepa kuzungumzia hayo wiki iliyopita akidai ana haraka na tangu hapo amekuwa hapokei simu pia.
0 comments:
Post a Comment