• HABARI MPYA

    Monday, October 13, 2014

    SIMBA SC WACHEZA NA WITS UNIVERSITY LEO, KESHO COSSMOS NA JUMATANO SUPERSPORT

    Na Princess Asia, JOHANNESBURG
    SIMBA SC asubuhi ya leo, inacheza mechi yake ya pili ya kujipima nguvu katika ziara yake ya Afrika Kusini, itakapomenyana na Wits University mjini Johannesburg.
    Simba SC ambayo imeweka kambi Afrika Kusini kujiandaa na mechi dhidi ya watani, Yanga SC Oktoba 18, Dar es Salaam, mchezo wa kwanza ilitoa sare ya bila kufungana na Orlando Pirates Jumamosi asubuhi.
    Katika mchezo huo, Simba SC itaendelea kuwakosa wachezaji wake, mshambuliaji Mganda, Emmanuel Okwi aliyekuwa na timu yake ya taifa, Uganda na mabeki Miraji Adam na Joram Mgeveke na viungo Jonas Mkude, Amri Kiemba, Said Ndemla na Haruna Chanongo waliokuwa na timu yao ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars. 
    Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba SC, Zacharia Hans Poppe kulia akijadiliana jambo na kocha Patrick Phiri baada ya mazoezi ya jana asubuhi 

    Baada ya nyota hao kuiongoza Stars kuichapa Benin mabao 4-1, walitarajiwa kuondoka Alfajiri ya leo kwa Ndege ya Shirika la Afrika Kusini kwenda kuungana na wenzao.
    Lakini nyota hao wote wanatarajiwa kuichezea Simba SC katika mchezo wa tatu wa kujipima nguvu dhidi ya Jomo Cossmos na Jumatano dhidi ya SuperSport United.
    Simba SC inatarajiwa kurejea Dar es Salaam Ijumaa tayari kwa mchezo huo wa mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya mahasimu hao wa jadi, Yanga SC.
    Baada ya kutoa sare mechi zake zote tatu za awali Ligi Kuu, 2-2 na Coastal Union, 1-1 mara mbili na Polisi Moro na Stand United, Simba SC imepania kushinda mechi ya kwanza Jumapili wiki hii.
    Orlando Pirates wakiingia uwanjani kucheza na Simba SC juzi 
    Wachezaji wa Simba SC wakiwasili Orlando Pirates
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SIMBA SC WACHEZA NA WITS UNIVERSITY LEO, KESHO COSSMOS NA JUMATANO SUPERSPORT Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top