• HABARI MPYA

    Sunday, October 12, 2014

    RONALDO 'ATOKOTA' URENO IKILAMBWA 2-1 NA UFARANSA

    UFARANSA imeifunga Ureno mabao 2-1 katika mchezo wa kirafiki wa kimatafa, ambao MwanasokamBora wa Dunia Cristiano Ronaldo hakuumaliza baada ya kuumia.
    Ronaldo alikwenda benchi dakika ya 76 na kufungwa barafu kwenye goti, wakati huo Ufaransa inaongoza kwa mabao 2-0. 
    Mabao hayo yalifungwa na mchezaji mwenzake wa 
    Real Madrid, Karim Benzema dakika ya tatu na mchezaji mwenzake wa zamani wa Manchester United, Paul Pogba dakika ya 65. 
    Ricardo Quaresma aliyetokea benchi aliwafungia bao la kufutuia machozi wageni dakika ya 78 kwa penalti.
    Cristiano Ronaldo katikati ya Paul Pogba na Sagna jana  
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: RONALDO 'ATOKOTA' URENO IKILAMBWA 2-1 NA UFARANSA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top