Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
KAMATI ya Nidhamu ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), imemfungia kwa miaka saba, Dk Damas Ndumbaro kujihusisha na masuala ya soka ndani na nje ya nchi.
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Nidhamu, Jerome Msemwa amewaambia Waandishi wa Habari leo mjini Dar es Salaam kwamba, Ndumbaro amekutwa na makosa mawili.
Amesema baada ya kikao cha siku mbili mwishoni mwa wiki, Ndumbaro amefungiwa mwaka mmoja kwa kosa la kwanza kutoa taarifa zisizo sahihi kiasi cha kupotosha mamuzi ya TFF kinyume cha kanuni nambari 41 kifungu kidogo cha sita cha kanuni za Ligi toleo la mwaka 2014.
Aidha, Wakili huyo pia amefungiwa miaka saba kwa kosa la pili, ambalo ni kushawishi au kupotosha na kuzuia maamuzi ya TFF kupitia bodi ya Ligi kinyume cha kanuni ya nne kifungu kidogo cha 16 toleo la mwaka 2014.
Hata hivyo, Msemwa amesema pamoja na kwamba adhabu ya jumla inakuwa miaka nane, lakini Ndumbaro atatumikia adhabu hiyo kwa miaka saba, kwa kuwa mwaka mmoja upo ndani ya miaka saba.
Akifafanua, Msemwa alisema kwamba Wakili Ndumbaro akiwa mwanafamilia wa TFF kwa vyeo vyake vya Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya klabu ya Simba na Mjumbe wa Bodi ya Ligi, alikubali kuziwakilisha klabu dhidi ya TFF.
Alisema kufanya hivyo ni makosa kwa sababu yeye yumo ndani ya TFF na maana yake anajua siri za shirikisho, kwa hivyo alichotakiwa ni kukataa.
Alisema pia, Ndumbaro aliupotosha umma kwa kusema klabu 12 zilimuomba kuwawakilisha kupinga makato ya asilimia tano za fedha za udhamini wa Ligi Kuu, wakati klabu nyingine zilikana kuhusika na mpango huo, Coastal Union na Stand United.
Msemwa alisema kwamba pia Kamati yake ilitilia shaka kama klabu ya Yanga ilikubali kuwakilishwa na Ndumbaro kwa sababu anatoka kwa mahasimu wao, Simba SC.
Wakili Ndumbaro aliitwa kwenye kikao cha Kamati hiyo ya Nidhamu, lakini akasema hataweza kuhudhuria kwa sababu anasifiri nje ya nchi- lakini hiyo haikuizuia Kamati hiyo kukutana na kufikia maamuzi hayo.
Kupitia kampuni yake ya Uwakili ya Meleta & Ndumbaro, Ndumbaro alisema ametumwa na klabu kupinga juu ya mpango wa TFF kukata asilimia tano za fedha za udhamini za Ligi Kuu.
Ndumbaro ambaye ni Mjumbe wa Bodi ya Ligi wa kuteuliwa- aliwaandikia barua TFF kupitia kampuni yake ya uwakili, Meleta & Ndumbaro kuwazuia kukata asilimia tano ya fedha za udhamini wa Ligi Kuu kwa sababu ni kinyume cha mikataba ya Vodacom, wadhamini na akatishia kuitisha mkutano Mkuu wa kumng’oa Malinzi madarakani.

![]() |
Jerome Msemwa kushoto akizungumza na Waandishi wa Habari leo, kulia ni Mkurgenzi wa Uanachama wa TFF, Eliud Mvella |

0 comments:
Post a Comment