Na Prince Akbar, DAR ES SALAAM
WACHEZAJI saba wa klabu ya Yanga SC ya Dar es Salaam wanatarajiwa kuingia kambini leo katika kikosi cha timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars kinachojiandaa na mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya Benin mwishoni mwa wiki.
Yanga SC iliwazuia wachezaji wake saba kujiunga na Taifa Stars hadi Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) liwaandikie barua rasmi ya kuwaomba.
Wachezaji wa Yanga SC walioitwa Stars inayofundishwa na kocha Mholanzi, Mart Nooij ni kipa Deogratius Munishi ‘Dida’, mabeki Oscar Joshua, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Kelvin Yondani, Charles Edward na mawinga Simon Msuva na Mrisho Ngassa.
TFF imetekeleza agizo hilo la Yanga SC na sasa wachezaji hao watajiunga na wenzao leo kambini, hoteli ta Tansoma kwa ajili ya mchezo wa mwishoni mwa wiki ulio katika kalenda ya Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA).
Taifa Stars na Benin ‘Squirrels’ zitamenyana Oktoba 12, kuanzia Saa 11:00 jioni, mchezo ambao utatanguliwa na mechi ya kudumisha upendo, amani, udugu na ushirikiano kati ya timu za taasisi za dini ya Kiislamu na Kikristo itakayoanza Saa 9:00 Alasiri.
Kikosi kamili cha Stars kilichoteuliwa kwa ajili ya mchezo huo ni; ni makipa Deogratias Munishi (Yanga), Aishi Manula (Azam), na Mwadini Ali (Azam).
Mabeki ni Gardiel Michael (Azam), Said Moradi (Azam), Shomari Kapombe (Azam), Oscar Joshua (Yanga), Nadir Haroub (Yanga), Kelvin Yondani (Yanga), Aggrey Morris (Azam), Miraji Adam (Simba), Joram Mgeveke (Simba), Charles Edward (Yanga) na Emmanuel Simwanda (African Lyon).
Viungo ni Jonas Mkude (Simba), Erasto Nyoni (Azam), Mwinyi Kazimoto (Al Markhiya, Qatar), Amri Kiemba (Simba), Himid Mao (Azam), Salum Abubakar (Azam), Said Ndemla (Simba) na Haruna Chanongo (Simba).
Washambuliaji ni Khamis Mcha (Azam), Simon Msuva (Yanga), Thomas Ulimwengu (TP Mazembe, DR Congo), Mbwana Samata (TP Mazembe, DR Congo), Mrisho Ngasa (Yanga), Mwegane Yeya (Mbeya City), na Juma Liuzio (Zesco, Zambia).

![]() |
Wachezaji wa Yanga kutoka kulia Oscar Joshua, Nadir Haroub 'Cannavaro' na Simon Msuva |

0 comments:
Post a Comment