MSHAMBULIAJI Robbie Keane amefunga mabao matatu peke yake Jamhuri Ireland ikishinda 7-0 dhidi ya Gibraltar katika mchezo wa Kundi D kufuzu Euro 2016.
Keane alifunga mabao yake katika dakika za sita, 14 na 18 kwa penalti, wakati James McClean alifunga mawili dakika za 46 na 53, huku kipa wa Gibraltar, Jordan Perez akijifunga dakika ya 52 na Wesley Hoolahan akahitimisha sherehe hiyo ya mabao dakika ya 56.
Mechi za kundi F, Romania imetoka 1-1 na Hungary sawa na Finland na Ugiriki, wakati Ireland Kaskazini imeichapa Faroe Islands 2-0 na Kundi I, Armenia imetoka 1-1 na Serbia sawa na Albania na Denmark.
0 comments:
Post a Comment