• HABARI MPYA

    Saturday, October 11, 2014

    UGANDA YAFUMULIWA 1-0 NA TOGO NYUMBANI KUFUZU AFCON, SUDAN WAWAKALISHA MABINGWA WA AFRIKA

    UGANDA, The Cranes imefungwa 1-0 na Togo katika mchezo wa Kundi E kufuzu Fainali za Mataifa ya Afrika mjini Kampala, Uganda leo.
    Bao lililoizamisha Uganda jioni ya leo limefungwa na 
    Donou Kokou dakika ya 30 na matokeo hayo yanaifanya Togo ibebe pointi tatu za kwanza baada ya awali kupoteza mechi mbili, wakati Cranes inabaki na pointi zake nne.
    Ghana inayomenyana na Guinea leo inaweza kuendelea kuwa kileleni ikishinda, kwani itatimiza pointi saba.
    Katika mechi nyingine za leo kufuzu AFCON ya mwakani Morocco, Gabon imeilaza 2-0 Burkina Faso, mabao ya Pierre-Emerick Aubameyang dakika ya 67 na 74 mjini Libreville, Sudan imewafunga mabingwa watetezi, Nigeria 1-0, bao pekee la Bakri Abd Elgadir dakika ya 41.
    Niger imetoka sare ya 0-0 na Zambia, Kongo imefungwa 2-0 nyumbani na Afrika Kusini, mabao ya Bongani Ndulula dakika ya 52 na Tokelo Anthony Rantie dakika ya 55, wakati DRC imefungwa 2-1 nyumbani na Ivory Coast. Bao la DRC limefungwa na Cedric Mongongu dakika ya 71, wakati mabao ya Tembo yamefungwa na Wilfred Bony dakika ya 23 na Max Gradel dakika ya 83.
    Msumbiji imeifunga 2-0 Cape Verde, mabao ya Saddan Guambe dakika ya 43 na Artur Faife dakika ya 60, wakati Sierra Leone imetoka sare 0-0 na Cameroon na Ethiopia imefungwa 2-0 nyumbani na Mali mabao ya Abdoulay Diaby dakika ya 33 na Sambou Yatabare dakika ya 60.
    Malawi imefungwa 2-0 nyumbani na Algeria mabao ya Rafik Halliche dakika ya 10 na Saphir Taider dakika ya 93. Katika mechi za jana Senegal ilitoka 0-0 na Tunisia sawa na Lesotho na Angola, wakati Botswana ilifungwa 2-0 nyumbani na Misri mabao ya Mohamed El Nenny dakika ya 56 na Mohamed Salah dakika ya 61. Mechi za marudiano zitachezwa Jumatano zikiwa ni za kwanza katika mzunguko wa pili.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: UGANDA YAFUMULIWA 1-0 NA TOGO NYUMBANI KUFUZU AFCON, SUDAN WAWAKALISHA MABINGWA WA AFRIKA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top