• HABARI MPYA

    Sunday, October 05, 2014

    MAFUNZO YA USAJILI LIGI DARAJA LA PILI

    Na Boniface Wambura, DAR ES SALAAM
    SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) litaendesha mafunzo ya usajili kwa klabu za Ligi Daraja la Pili (SDL) yatakayofanyika kesho na keshokutwa (Oktoba 6 na 7 mwaka huu) kwenye hosteli ya TFF iliyopo Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume kuanzia saa 3 asubuhi.
    Mafunzo hayo yatahusu usajili wa mtandao ambao ndiyo klabu hizo zitautumia kwa ajili ya Ligi hiyo itakayoanza baadaye mwezi ujao katika makundi manne ya timu sita sita kwa mtindo wa nyumbani na ugenini.

    Kesho mafunzo hayo yatakuwa kwa ajili ya maofisa wa usajili wa klabu za Abajalo, Arusha FC, Kiluvya United, Magereza Iringa, Milambo SC, Mji Mkuu (CDA), Mkamba Rangers, Mshikamano, Mvuvumwa FC, Navy, Njombe Mji, Singida United, Transit Camp, Volcano FC na Wenda FC.
    Oktoba 7 mwaka huu mafunzo hayo yatahusisha maofisa usajili wa klabu za Bulyanhulu FC, Eleven Stars, JKT Rwamkoma, Kariakoo Lindi, Mbao FC, Mpanda United, Pamba, Town Small Boys na Ujenzi Rukwa.
    Wakati huo huo: TFF imefanya mabadiliko kwa baadhi ya mechi za kundi B Ligi Daraja la Kwanza (FDL) baada ya kupokea barua kutoka Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Mwanza (MZFA) ikieleza kuwa Uwanja wa CCM Kirumba utatumika kwa shughuli za kidini kuanzia Oktoba 16 hadi 19 mwaka huu.
    Kutokana na hali hiyo, mechi namba 17 kati ya Toto Africans na Green Warriors iliyokuwa ichezwe kwenye uwanja huo Oktoba 18 mwaka huu sasa itafanyika Oktoba 20 mwaka huu.
    Mabadiliko hayo pia yameathiri mechi namba 19 kati ya Green Warriors na Oljoro JKT ambayo sasa itachezwa Uwanja wa Karume, Dar es Salaam, Oktoba 23 mwaka huu badala ya Oktoba 21 mwaka huu.
    Vilevile mechi namba 25 kati ya Burkina Faso na Oljoro JKT imesogezwa mbele kwa siku moja kutoka Oktoba 25 mwaka huu hadi Oktoba 26 mwaka huu. Mechi hiyo itachezwa Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MAFUNZO YA USAJILI LIGI DARAJA LA PILI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top