• HABARI MPYA

    Tuesday, October 07, 2014

    KENYA YAPITISHWA KUGOMBEA UENYEJI WA AFCON 2017

    Na Prince Akbar, DAR ES SALAAM
    KENYA ni kati ya nchi saba ambazo zimepitishwa na Shirikisho la Soka Afrika (CAF) kugombea kuandaa Fainali za Mataifa ya Afrika 2017.
    Wakati tarehe ya mwisho ya kuomba ilikuwa Septemba 30, mwaka huu- maombi yaliyopokelewa ni ya Algeria, Misri, Gabon, Ghana, Kenya, Sudan na Zimbabwe, huku Tanzania ikiwa ni moja ya nchi zilizokataliwa kwa sababu haijawahi kuandaa fainali za vijana kabla.

    Maombi yalifunguliwa Agosti 23 mwaka 2014, kufuatia kujitoa kwa Libya, waliopewa uenyeji wa fainali hizo za 31.
    Katibu Mkuu wa CAF, Hicham El Amrani alitangaza rasmi kusaka nchi ya kuchukua nafasi ya Libya na baada ya nchi saba kujitokeza, mwenyeji atateuliwa na kikao cha Kamati Kuu ya CAF mapema mwakani.
    CAF itatoa kipaumbele kwa nchi yenye miundombinu bora, ikiwa ni pamoja na viwanja vyenye ubora kwa ajili ya mazoezi na mechi.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: KENYA YAPITISHWA KUGOMBEA UENYEJI WA AFCON 2017 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top