• HABARI MPYA

    Tuesday, October 07, 2014

    MCHEZAJI ZIMAMOTO AFUNGIWA MECHI TATU LIGI KUU ZENJI KWA KUINGIZA NDONDI KWENYE SOKA

    Na Ally Cheupe, ZANZIBAR
    KLABU ya Zimamoto inayoshiriki Ligi Kuu ya soka ya Grand Malt Zanzibar imezidi kupata doa kufuatia mchezaji wake Ali Salum Bakar maarufu Kibata (pichani chini) kufungiwa kutoshuka kiwanjani kwa michezo mitatu.
    Kifungo hicho kimetolewa na Chama cha Soka (Zanzibar) ZFA kufuatia mwanandinga huyo kumpiga ngumi kiwanjani mchezaji wa timu ya Malindi, Abdallah Said Hamad kitendo kilichosababisha kutolewa nje kwa kuonyeshwa kadi nyekundu.

    kwa mujibu wa kanuni ya kuendeshea ligi kuu ya soka Zanzibar kifungu cha 16 c "Mchezaji atakaetolewa nje kwa kadi nyekundu kwa kosa la kupiga au kupigana atakaa nje na kutocheza michezo mitatu(3) inayofuata ya klabu yake pamoja na kulipa faini ya shilingi elfu hamsini (50,000/)
    Klabu hiyo ya Zimamoto tayari imeshapata aibu kutokana na rekodi za mchezaji huyo kwani kwenye pambano la ufunguzi wa ligi September 15, 2014 dhidi ya timu ya Chuoni pia alionyeshwa kadi nyekundu.
    Ali ambaye alipata tuzo ya mchezaji bora kwa msimu wa ligi 2013/2014 alisajiliwa na Zimamoto akitokea timu ya Mtende Rangers kawenye kipindi cha uhamisho na Usajili kilichoishia mwezi Agost mwaka huu.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MCHEZAJI ZIMAMOTO AFUNGIWA MECHI TATU LIGI KUU ZENJI KWA KUINGIZA NDONDI KWENYE SOKA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top