• HABARI MPYA

    Tuesday, October 07, 2014

    HOMA YA PAMBANO NA YANGA; SIMBA SC WAENDA KUWEKA KAMBI AFRIKA KUSINI KESHO

    Na Princess Asia, DAR ES SALAAM
    SIMBA SC inaweza kuondoka kesho nchini kwenda kuweka kambi Afrika Kusini kwa ajili ya mpambano na mahasimu wao, Yanga SC Oktoba 18, mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
    Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba SC, Zacharia Hans Poppe yuko Cape Town tangu jana na kikosi kinaweza kuondoka kesho na kurejea Dar es Salaam siku moja kabla ya mechi na watani.
    Wacheaji waliopo timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars wataondoka Dar es Salaam baada ya mechi na Benin Jumatatu.
    Hans Poppe yuko Cape Town tangu jana na Simba SC inatarajiwa kwenda Afrika Kusini kesho

    Mshambuliaji Mganda, Emmanuel Okwi hatakwenda kabisa Afrika Kusini kwa sababu atakuwa kwenye majukumu ya kimataifa kwao, Uganda. 
    Kutwa nzima ya leo, uongozi wa Simba SC ulikuwa unawashughulikia baadhi ya wachezaji ambao hawana pasipoti ili kuhakikisha wanakuwemo kwenye safari kesho.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: HOMA YA PAMBANO NA YANGA; SIMBA SC WAENDA KUWEKA KAMBI AFRIKA KUSINI KESHO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top