Na Samira Said, DAR ES SALAAM
WAKATI Kamati ya Uchaguzi ya Klabu ya Simba jana imetangaza rasmi kuwatema wanachama saba waliokuwa wanawania nafasi ya Ujumbe wa Kamati ya Utendaji ya klabu hiyo wengine watano wameandika barua za kujiondoa kwenye kinyang'anyro hicho imeelezwa.
Akizungumza leo mjini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya klabu hiyo, Damas Ndumbaro, aliwataja wagombea walioondolewa katika mchakato wa uchaguzi kwa sababu ya sifa za kutokuwa na elimu ya kidato cha nne iliyothibitishwa na Baraza la Mitihani Nchini kama ilivyoelezwa katika katiba ibara ya 26(2) ni pamoja na George Wakuganda, Salim Jazaar na Sueliman Dewji.
Ndumbaro aliwataja wagombea waliotema kutokana na uanachama wao kutotimia miaka mitatu na kuruhusiwa kugombea kwa mujibu wa ibara ya 26( 6) cha katiba ya Simba ni Emmanuel Kazimoto, Ahmed Mlanzi, Omary Omary na Ramson Rutiginga.
Aliwataja wagombea waliojiondoa kwa sababu za kifamilia na kuwasilisha barua kwa kamati hiyo ni Juma Pinto, Asha Kigundula, na Hussein Simba waliokuwa wanawania Ujumbe wa Kamati ya Utendaji na kwenye nafasi ya Makamu wa Rais ni Joseph Itang'are na Wilbroad Mayage.
Aliwataja wagombea waliopitishwa kuwa ni Evans Aveva na Andrew Tupa (Urais) na Geofrey Nyange 'Kaburu', Swedy Mkwabi, Jamhuri Kihwelo 'Julio' na Bundala Kaburwa wanaowania nafasi ya Makamu wa Rais.
Nafasi ya Ujumbe ni Ally Suru, Abdulhamid Mshangama, Alfred Elia, Chano Almasi, Amina Poyo, Asha Muhaji, Collins Frisch, Ally Chaurembo, Daniel Manembe, Khamis Mkoma, Iddi Mkambala, Addi Kajuna, Jasmin Badar, Juma Mussa, Maulid Abdallah, Rodney Chiduo, Said Kubenea, Said Pamba, Said Tully na Yasin Mwete.
Hata hivyo Ndumbaro alisema kwamba hiyo si orodha ya mwisho ya wagombea kwa sababu sasa hivi kamati yake inapeleka majina hayo katika Kamati ya Maadili kwa ajili ya kuyapitisha.
"Orodha ya mwisho itatolewa Juni 23, huenda majina mengine kati ya haya yanaweza kukumbwa na Kamati ya Maadili ya TFF au mamlaka husika za dola ambazo bado wanendelea na kazi zao, tunachotaka haki sio itendeke, bali ionekane imetendeka," alisema Ndumbaro.
Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa na kamati hiyo, kuanzia leo hadi Juni 7 ni muda wa Kamati ya Rufaa kukutana kujadili pingamizi au rufaa zitakazokuwa zimewasilishwa.

![]() |
Dk Damas Ndumbaro kulia akizungumza |

0 comments:
Post a Comment