Na Samira Said, DAR ES SALAAM
UONGOZI wa Klabu ya Yanga umesema kuwa utahakikisha mshambuliaji wa kimataifa wa timu hiyo kutoka Uganda, Emmanuel Okwi, ataichezea timu yao katika msimu ujao wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara na mashindano ya kimataifa.
Akizungumza katika mkutano wa wanachama uliofanyika leo kwenye Ukumbi wa Bwalo la Maafisa wa Polisi Oysterbay, Mwenyekiti wa Klabu hiyo, Yusuph Manji, alisema kuwa uongozi uko katika mazungumzo na mchezaji huyo ili aweze kurejea kuitumikia Yanga kwa sababu ni mali yao.
Kiongozi huyo alisema kwamba endapo mazungumzo na Okwi yatashindikana, Yanga itahakikisha inasajili mchezaji mwingine mwenye uwezo wa juu kuliko nyota huyo wa zamani wa Simba ili kuimarisha kikosi chao.
"Tutahakikisha tunafanya juu chini Okwi anarejea Yanga na endapo itashindikana, tutaleta mchezaji mwingine mbadala mwenye uwezo zaidi yake," alisema kiongozi huyo.
Alieleza kwamba Yanga imebakiza nafasi tano za kusajili na kati ya hizo, tatu ni za wachezaji wa ndani na mbili za wachezaji kutoka nje ya nchi.
Okwi alianza kuikacha Yanga kwa madai kwamba anataka amaliziwe kiasi cha Dola za Marekani 50,000 ambazo alikuwa anadai kutokana na makubaliano na uongozi wakati anasaini mkataba.
UJENZI WA UWANJA
Katika mkutano huo uliotishwa kwa lengo la kufanya mabadiliko ya katiba, wanachama wa Yanga walielezwa kwamba tayari Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mecky Sadick, ameshatoa ruhusa ya kuongezewa eneo lakini kizuizi kimebaki kwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala.
Wanachama wa Yanga walielezwa kwamba bado uongozi wa klabu hiyo haujakata tamaa na wanaendelea na juhudi za kuomba eneo zaidi la ujenzi licha ya kukwamishwa kwa zaidi ya miezi 19 tangu walipopeleka maombi yao.

![]() |
Emmanuel Okwi kulia. Manji amesema mchezaji huyo wa Uganda hataondoka Yanga SC |

0 comments:
Post a Comment