// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); STARS YAMTIMUA KOCHA WA ZIMBABWE - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE STARS YAMTIMUA KOCHA WA ZIMBABWE - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Tuesday, June 03, 2014

    STARS YAMTIMUA KOCHA WA ZIMBABWE

    Na Mahmoud Zubeiry, HARARE
    KOCHA wa Zimbabwe, Mzalendo Ian Gorowa amebwaga manyanga baada ya kutolewa na Tanzania katika mbio za Mataifa ya Afrika 2015 nchini Morocco.
    Taifa Stars imesonga mbele katika hatua ya mwisho ya mchujo kuwania kupangwa kwenye makundi ya kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Mataifa ya Afrika mwakani Morocco, baada ya sare ya 2-2 na Zimbabwe Jumapili Uwanja wa Taifa, Harare. 
    Amerusha taulo; Kocha wa Zimbabwe juzi Uwanja wa Taifa wa Harare alibadilisha kila aina ya mikao kuiongoza timu yake, lakini bahati haikuwa yao mbele ya vijana wa Tanzania

    Kwa matokeo hayo, Stars imefuzu kwa ushindi wa jumla wa mabao 3-2, baada ya ushindi wa awali wa 1-0 wiki iliyopita Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam bao pekee la John Bocco.
    Stars ambayo mabao yake ya juzi yalifungwa na Nahodha Nadir Haroub ‘Cannavaro’ na Thomas Ulimwengu, sasa itamenyana na Msumbiji mwezi ujao katika hatua ya mwisho ambako ikifuzu itaingia kwenye kundi kuanza rasmi mbio za Morocco mwakani.
    Gazeti la H-Metro la hapa jana limeandika kwamba Gowowa alitamka maneno mazito kwa wachezaji wake juzi baada ya mechi chumbani na akasema haoni faida ya kuendelea kuifundisha timu hiyo kama matokeo mazuri hayapatikani.
    Pia, aliwalaumu sana wachezaji wake kwa kushindwa kucheza vizuri na kuruhusu sare hiyo ya nyumbani.
    Lakini Msemaji wa Chama cha Soka Zimbabwe (ZIFA), Xolisani Gwesela alisema hawajapata taarifa rasmi ya kocha huyo kujiuzulu na watakuwa tayari kuzungumza mara watakapoipata. 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: STARS YAMTIMUA KOCHA WA ZIMBABWE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top