// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); NIGERIA YATEMA SABA KIKOSI CHA MWISHO KOMBE LA DUNIA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE NIGERIA YATEMA SABA KIKOSI CHA MWISHO KOMBE LA DUNIA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Tuesday, June 03, 2014

    NIGERIA YATEMA SABA KIKOSI CHA MWISHO KOMBE LA DUNIA

    Na Mwandishi Wetu, LAGOS
    NIGERIA imewatema wachezaji saba wakiwemo Sunday Mba, Nosa Igiebor na Ejike Uzoenyi katika kikosi chake cha mwisho cha Kombe la Dunia.
    Taarifa ya Shirikisho la Soka Nigeria (NFF) imesema kwamba kipa wa Warri Wolves, Daniel Akpeyi, Joel Obi, Obinna Nsofor na Nnamdi Oduamadi pia hawatakuwamo katika kikosi cha wachezaji 23 kitakachokwenda Brazil, baada ya kutemwa na kocha Stephen Keshi.
    Sunday Mba ametemwa

    Keshi amechukua mabeki tisa, viungo watano na washambuliaji saba pamoja na makipa watatu.
    Mabingwa hao wa Afrika wataanza kampeni zao Juniu 16 kwa kumenyana na Iran.
    Kikosi kamili ni, makipa; Vincent Enyeama, Austin Ejide na Chigozie Agbim, mabeki; Joseph Yobo, Elderson Echiejile, Juwon Oshaniwa, Godfrey Oboabona, Azubuike Egwuekwe, Kenneth Omeruo, Efe Ambrose na Kunle Odunlami.
    Viungo ni; John Obi Mikel, Ogenyi Onazi, Ramon Azeez, Michael Uchebo na Reuben Gabriel, wakati washambuliaji ni Peter Odemwingie, Ahmed Musa, Shola Ameobi, Emmanuel Emenike, Babatunde Michael, Victor Moses na Uche Nwofor.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: NIGERIA YATEMA SABA KIKOSI CHA MWISHO KOMBE LA DUNIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top