// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); MSIBA, KIONGOZI TFF AFARIKI DUNIA MARA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE MSIBA, KIONGOZI TFF AFARIKI DUNIA MARA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Tuesday, June 03, 2014

    MSIBA, KIONGOZI TFF AFARIKI DUNIA MARA

    Na Boniface Wambura, DAR ES SALAAM
    SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limepokea kwa masikitiko kifo cha Mwakilishi wa Chama cha Soka Mara (FAM) katika Mkutano Mkuu wa TFF, William Chibura kilichotokea leo asubuhi (Juni 3 mwaka huu) katika Hospitali ya Mkoa wa Mara mjini Musoma.
    Chibura aliyezaliwa mwaka 1969 alikuwa mjumbe wa Mkutano Mkuu wa TFF akiwakilisha klabu za Mkoa wa Mara kupitia FAM. Aliwahi kuichezea Musoma Shooting, na baadaye kuwa kiongozi katika klabu hiyo na ile ya Polisi Mara iliyoko Ligi Daraja la Kwanza (FDL).
    William Chibura enzi za uhai wake akiwa na Kombe la Dunia la FIFA lilipofanya ziara nchini 

    Hadi mauti yanamkuta alikuwa kiongozi wa Butiama FC, na mwakilishi wa klabu Chama cha Mpira wa Miguu Wilaya ya Butiama (MUFA) kwenye Mkutano Mkuu wa FAM.
    TFF imesema msiba huo ni mkubwa katika familia ya soka nchini, kwani Chibura enzi za uhai wake alitoa mchango mkubwa katika mchezo huu tangu akiwa mchezaji na baadaye kiongozi.
    TFF inatoa pole kwa familia ya marehemu Chibura, Jeshi la Polisi Tanzania na kuwataka kuwa na subira na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu cha msiba huo mzito.
    Taratibu za mazishi zinaendelea kufanywa na familia yake kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi Tanzania- Mkoa wa Mara, kwani marehemu Chibura alikuwa mtumishi wa jeshi hilo. TFF inasubiri taratibu hizo ili waweze kujipanga jinsi ya kushiriki katika msiba huo.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MSIBA, KIONGOZI TFF AFARIKI DUNIA MARA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top