KLABU ya Liverpool inajiandaa kumsajili Emre Can kutoka Bayer Leverkusen baada ya kuwa tayari kutoa dau la Pauni Milioni 9.75 ambalo ndilo thamani ya mkataba wake.
Kocha Brendan Rodgers amekuwa akimfukuzia mcheaji huyo wa timu ya vijana ya Ujerumani chini ya umri wa miaka 21 kwa muds mrefu na sasa yuko tayari kumchukua.
Kiungo huyo mtaalamu wa kusambaza mipira kutokea eneo la katikati ya Uwanja mwenye umri wa miaka 20 anaweza kuwaongezea ubora Wekundu hao wa Anfield akisajiliwa.



.png)
0 comments:
Post a Comment