// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); HILI LIWE FUNDISHO KUBWA KWA TFF, SIMBA NA YANGA...SOKA NI MCHEZO WA WALALAHOI - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE HILI LIWE FUNDISHO KUBWA KWA TFF, SIMBA NA YANGA...SOKA NI MCHEZO WA WALALAHOI - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Tuesday, June 03, 2014

    HILI LIWE FUNDISHO KUBWA KWA TFF, SIMBA NA YANGA...SOKA NI MCHEZO WA WALALAHOI

    Na Mahmoud Zubeiry, HARARE
    CHAMA cha Soka Zimbabwe juzi kiliweka kiingilio cha dola ya Kimarekani 1, sawa na Sh. 1,600 ya Tanzania katika mchezo dhidi ya Taifa Stars Jumapili kuwania tiketi ya Fainali za Mataifa ya Afrika mwakani Uwanja wa Taifa wa Harare.
    Na Wazimbabwe walijitokeza kwa wingi na kuujaza Uwanja kuishangilia timu yao katika mchezo huo muhimu. 
    Bahati mbaya kwao, walilazimishwa sare ya 2-2 na kutolewa kwa jumla ya mabao 3-2 baada ya awali kufungwa 1-0 Dar es Salaam. 
    Dola 1 hajivungi mtu; Wazimbabwe waliujaza Uwanja kwa kiingilio nafuu cha dola 1 ya Kimarekani

    Wananchi wa hapa wanaushutumu uongozi wa ZIFA ni mbovu umesababisha matokeo hayo. ZIFA wanalaumiwa hata kwa makosa ya ball boys (vijana waokota mipra) kurusha mipira uwanjani wakati mwingine upo, hivyo kusababisha mchezo kuchelewa kuendelea wakati Worries wanasaka mabao.
    Mwandishi Charles Mushinga ameandika kwenye gazeti la H- Metro akisema wachezaji walikuwa wanapewa posho ya dola 15 (kama Sh. 25,000 ya Tanzania) kwa siku na kwa sababu hiyo hastaajabiswhi na matokeo hayo, kwani posho ndogo wachezaji hawawezi kujituma.
    Kwa sasa ni wakati mgumu kwa ZIFA na wachezaji wa Zimbabwe baada ya matokeo ya Jumapili. Tunawaachia ZIFA na Wazimbabwe matatizo yao, lakini kwa mazuri lazima tuyachukue.
    Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam umekumbwa na uhaba wa mashabiki katika michezo kuanzia ya timu za taifa hadi klabu kubwa wakati wa hatua ya mwisho ya Ligi Kuu.
    Yanga SC ilikuwa inaingiza mashabiki wengi uwanjani hadi baada ya mechi na Al Ahly Ligi ya Mabingwa na hata katika mechi yao na Azam watu walijitokeza kwa wingi.
    Ila baada ya kufungwa na Mgambo Tanga, kwa kurejea sare na Azam FC na Mtibwa Sugar, watu wa Yanga wakaamua kuwa wanaangalia mpira kwenye Televisheni.
    Kama mashabiki wa Tanzania wameweza kusafiri hadi Harare kuisapoti timu, wanaweza kujitokeza kwa wingi hata Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Ipo haja ya kupunguza viingilio. 

    Waende kushangilia timu ipi iliyopoteza pointi kwa urahisi katika mechi tatu mfululizo? Simba SC ilipoteza mvuto kwa mashabiki wake mapema tu baada ya kupotea mwelekeo.
    Matokeo mabaya mfululizo ya Taifa Stars siku za karibuni chini ya kocha aliyefukuzwa, Mdenmark Kim Poulsen yaliwafukuza mashabiki uwanjani. 
    Mechi zote za timu za taifa kwa sasa watu hawaendi kwa wingi uwanjani- na wazi Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) linakuwa na mzigo mzito wa kuweza kuzihudumia timu hizo haswa za vijana, ambazo hazina udhamini ikiwa hata mapato hayapatikani milangoni.
    Lakini bado pamoja na hali hiyo, TFF imeendelea kufanya Sh. 5,000 kuwa kiingilio cha chini katika mechi zote Uwanja wa Taifa. Timu hazifanyi vizuri, bado kiingilio kikubwa, kuna ajabu gani mashabiki kutojitokeza uwanjani.
    Mashabiki walifurika Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam wakati Azam FC ikimenyana na JKT Ruvu katika mechi ya mwisho ya Ligi Kuu siku ambayo pia watani wa jadi, Simba na Yanga walikuwa wanamenyana Uwanja wa Taifa.
    Watu hawakuwa wengi kwa kawaida ya mechi za watani wa jadi Uwanja wa Taifa, kwa sababu haikuwa mechi yenye maana yoyote na timu hizo zilikuwa zimekwishapoteza mvuto kwa mashabiki wake.
    Lakini bado kiingilio kingekuwa cha chini, watu wangeamua kwenda tu uwanjani japo kupoteza muda, ila TFF wakaweka viingilio vya juu na mechi ikawa na mapato haba.
    Ndiyo, tumewatoa Zimbabwe, lakini lazima tukubali ni timu bora kuliko sisi na ina wachezaji bora kuliko wetu, sema tu wakati mwingine soka ni mchezo wa bahati.
    Pamoja na ubora wa timu yao na wachezaji wao wakiwemo wanaocheza Afrika Kusini na Kaskazini mwa Afrika, bado kwenye mechi na Stars kiingilio kilikuwa dola 1.
    Sisi ambao tuna wachezaji wawili tu wanaocheza timu kubwa nje, Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu wa TP Mazembe mechi zetu tunaweka viingilio vikubwa vya kuwakatisha tamaa watu.
    Soka inapendwa zaidi na watu wa hali ya chini na lazima ifike wakati TFF ilizingatie hilo na kuweka kando tamaa ya kuweka viingilio vikubwa.
    Bora yale maeneo ya VIP ndiyo waweke viingilio vikubwa, hata 100,000 kwa tiketi, lakini kule kwa wapiga yowe uwanjani kuhamaisha wachezaji, viingilio viwe vya chini mno.
    Kama TFF itaamua kuanzia sasa kiingilio cha chini Uwanja wa Taifa, kiwe japo Sh. 2,000 tu, watu watafurika uwanjani, lakini wakiendelea na tamaa ya kuweka viingilio vikubwa, hali itaendelea kuwa ile ile.   
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: HILI LIWE FUNDISHO KUBWA KWA TFF, SIMBA NA YANGA...SOKA NI MCHEZO WA WALALAHOI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top