Tuesday, June 03, 2014

    AFC LEOPARDS NA VICTORY UNIVERSITY KUWANIA MILIONI 50 WALIZOZIKOSAKOSA MBEYA CITY

    Na Mwandishi Wetu, KHARTOUM
    AFC Leopards ya Kenya itamenyana na Victoria University ya Uganda katika Fainali ya michuano ya mipya ya Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki (CECAFA) Nile Basin kesho Uwanja wa Khartoum, Sudan.
    Hiyo inafuatia timu hiyo ya Uganda kuwatoa wenyeji, Al Shandy kwa bao 1-0 katika Nusu Fainali ya pili usiku wa jana Uwanja wa Khartoum, baada ya Leopards kuing’oa Academie Tchite kwa mabao 2-0.
    AFC Leopards ya Kenya itamenyana na Victory University kesho katika fainali ya Nile Basin 

    Victory University ndiyo walioitoa Mbeya City ya Tanzania kwa bao 1-0 katika Robo Fainali ya michuano hiyo inayofanyika kwa mara ya kwanza, ikishirikisha mabingwa wa FA wa nchi wanachama wa CECAFA, au washindi wa pili wa Ligi Kuu.
    Bingwa wa michuano hiyo, ataondoka na kitita cha dola za Kimarekani 30, 000 (Sh. Sh. Milioni 50 za Tanzania) na mshindi wa pili atabeba dola 20, 000 (Sh. Milioni 33).
    Mshindi wa tatu atakayepatikana katika mchezo baina ya Tchite na Shandy, ataondoka na dola 10 000 (Sh. Milioni 16.5).
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: AFC LEOPARDS NA VICTORY UNIVERSITY KUWANIA MILIONI 50 WALIZOZIKOSAKOSA MBEYA CITY Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry