// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); BREAKING NEWS; KOCHA MPYA BARCELONA AKIMBIZWA HOSPITALI, KUFANYIWA UPASUAJI LEO - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE BREAKING NEWS; KOCHA MPYA BARCELONA AKIMBIZWA HOSPITALI, KUFANYIWA UPASUAJI LEO - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Monday, June 09, 2014

    BREAKING NEWS; KOCHA MPYA BARCELONA AKIMBIZWA HOSPITALI, KUFANYIWA UPASUAJI LEO

    KOCHA wa Barcelona, Luis Enrique leo anatarajiwa kufanyiwa operesheni ya ugonjwa wa kidoletumbo.
    Kwa mujibu wa gazeti Mundo Deportivo la Hispania, mwalimu huyo mwenye umri wa miaka 44 alikimbizwa chumba cha dharula cha wagonjwa, kabla ya kwenda kufanyiwa vipimo kuthibitisha tatizo lake.
    Enrique, ambaye aliwachezea vigogo hao wa Hispania kuanzia mwaka 1996 hadi 2004, aliteuliwa kuwa kocha Mkuu wa Barcelona mwezi uliopita kwa Mkataba wa miaka miwili.

    Chini ya kisu: Kocha wa Barcelona, Luis Enrique leo atafanyiwa upasuaji wa kidoletumbo 

    Baada ya upasuaji huo, kocha huyo Mspanyola atahitaji kukaa nje muda mrefu kwa maumziko bila kuanya kazi.
    Enrique anaweza kuondoka hospital baada ya saa 24 iwapo mambo yatakwenda vizuri bila matatizo yoyote. 
    Kocha huyo wa zamani wa Celta Vigo atakuwa tayari kurejea kazini kwa ajili ya msimu mpya, iwapo mambo yatakwenda vizuri.
    Gerard Pique na Javier Mascherano waliosaini mikataba mipya hive karibuni kubaki katika klabu hiyo, wakati kiungo wa Sevilla, Ivan Rakitic yupo mbioni kutua Nou Camp.
    Enrique anatarajiwa kumpoteza Cesc Fabregas msimu ujao ambaye anatakiwa na Chelsea walio tayari kutoa Pauni  Milioni 30 kumchukua nyota huyo azibe pengo la Frank Lampard aliyeondoka baada ya kumaliza Mkataba.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: BREAKING NEWS; KOCHA MPYA BARCELONA AKIMBIZWA HOSPITALI, KUFANYIWA UPASUAJI LEO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top