Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
AZAM FC, imesema kwamba Simba SC inadanganywa na wakala Dennis Kadito kuhusu kiwango halisi cha manunuzi ya mchezaji Shomary Kapombe.
Azam FC imeiambia BIN ZUBEIRY leo kwamba, imemnunua Kapombe kwa Euro 43,000 kutoka AS Cannes ya Ufaransa na baada ya hapo, ikaelekezwa ilipe asilimia 20 ya dau hilo kwa wakala Kadito na asilimia 40 kwa Simba SC.
Azam FC imesema iko tayari kutekeleza hayo na imekwishaanza mchakato wa malipo, lakini tatizo lipo kwa Simba SC ambao wanadai fedha zaidi ya zile ambazo wanastahili kulipwa- kisa wanapotoshwa na Kadito.
Azam FC imesema awali katika mpango wa kumnunua Kapombe, iliwasiliana na Kadito, lakini akaonyesha kutaka fedha nyingi- hivyo wao wakaamua kwenda moja kwa moja AS Cannes.
“Kapombe ana Mkataba na AS Cannes, na sisi tumemnunua kutoka AS Cannes, ambao wao wana Mkataba na Simba SC. Cannes wametuelekeza cha kufanya baada ya hapo, na tuko tayari kuwalipa Kadito na Simba.
Ila kwa kuwa wao hawaamini kama kiwango tunachotaka ndicho tumeambiwa tuwape, milango ipo wazi kurudi Cannes kuthibitisha,”amesema mmoja wa Wakurugenzi wa Azam FC, ambaye hakupenda kutajwa jina.
Jana, Mwenyekiti wa Simba SC, Alhaj Ismail Aden Rage alisema hawawezi kupokea chini ya Euro 43,000 kutoka kwa Azam FC kutokana na uhamisho wa Kapombe.
Akizungumza na BIN ZUBEIRY jana, Rage alisema kwamba enzi za klabu hiyo kuuza wachezaji kwa dola za Kimarekani 10,000 zimepitwa na wakati chini ya viongozi ambao walikuwa si waelewa.
“Nasema, chini ya uongozi wangu, mtu yeyote asitegemee biashara ya chee, Azam wanamtaka Kapombe, walete Euro 43,000 vinginevyo hawatamtumia kwenye mashindano yoyote, watafanya naye mazoezi tu,”alisema Rage.
Rage amesema suala zima ka uhamisho wa Kapombe alilishughulikia Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya klabu hiyo, Zacharia Hans Poppe kwa ushirikiano naye wa karibu.
Amesema makubaliano yalikuwa kumpeleka Kapombe bure AS Cannes ya Ufaransa akaendelezwe ili baadaye auzwe klabu za Ulaya kwa bei nzuri, Simba SC inufaike.
“Na tulikubali hivyo baada ya wao wenyewe kutuonyesha kwenye tovuti yao namna wanavyouza wachezaji weusi kwa bei nzuri klabu za Ulaya. Hakuna mchezaji ambaye waliwahi kumuuza chini ya Euro Milioni 1.8,”amesema Rage.
Mbunge huyo wa Tabora Mjini (CCM) amesema kwa kujua hilo hawakuona sababu ya kuwa na tamaa ya kudai fedha mapema, wakaamua kuingia Mkataba na AS Cannes.
“Tukakubaliana wakifanikiwa kumuuza Kapombe popote, sisi watupe asilimia 40 ya bei waliyomuuza na wao wachukue asilimia 40, wakati asilimia 20 ni ya wakala wa Kapombe,”amesema Rage.
“Tulikuwa na imani kama Kapombe angebaki Ulaya na kuendelezwa, tungenufaika kwa sababu angeuzwa bei nzuri na Simba SC ingepata fedha nyingi,”.
Ilifikia wakati Kapombe akagoma kurudi Ulaya akidai hajalipwa mshahara wa mwezi mmoja, hadi ikabidi Hans Poppe ajitolee kumlipa huo mshahara huyu kijana ili arudi Ulaya, lakini mwenyewe akagoma,”
“Kwa kweli kitendo cha Kapombe kushindwa kurudi Ulaya kimetusikitisha sana, siyo tu kimetuharibia sisi kama klabu, bali kimewaharibia wachezaji wa Tanzania kwa ujumla,”.
“Wao (wachezaji wa Tanzania) wasione Waafrika wenzao wengine wanacheza timu kubwa Ulaya, kwa kweli wanaanzia mbali na wanakuwa wavumilivu na wenye malengo, ndiyo maana wanafanikiwa,”
“Sasa kwa Kapombe kugoma kurudi kule, maana yake kesho huwezi tena kumtafutia nafasi mchezaji wa Tanzania akafanikiwa, wamekwishatudharau,” amesema Rage.
Pamoja na yote, Rage amesema baada ya Kapombe kuamua kurudi Tanzania na kujiunga na Azam, Simba SC inataka taratibu zifuatwe ili wao wapate haki yao.
“Sisi tunazo hadi barua za Azam wamepeleka ofa ya Euro 40,000 ikakataliwa na Cannes. wakapeleka Euro 70,000 pia ikakataliwa. Sasa ambacho sisi tunaona hapa, ni kwamba Azam wamemnunua huyu mchezaji kwa Euro 107,000,”.
“Cannes wamepokea Euro 43, 000 ambayo ni asilimia 40 ya Euro 107,000. Maana yake na sisi Azam wanatakiwa kutupa kiwango hicho hicho. Lakini Azam wamemuandikia barua Katibu wangu wanasema wao wameambiwa na Cannes watulipe asilimia 40 ya Euro 43,000 kitu ambacho si sahihi na hatukubali,”amesema Rage.
Kapombe alikwenda Ufaransa katikati ya mwaka jana kujiunga na klabu hiyo ya Daraja la Nne, lakini Novemba mwaka huo aliporejea kuichezea Tanzania katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya Zimbabwe hakutaka tena kurudi Ulaya.
Machi mwaka huu, akaanza kufanya mazoezi na Azam FC kabla ya mwezi uliopita kusaini Mkataba wa miaka mitatu na mabingwa hao wapya wa Ligi Kuu nchini.

![]() |
Uhamisho wa Shomary kapombe kutoka AS Cannes umezua kizazaa Tanzania |

0 comments:
Post a Comment