• HABARI MPYA

    Monday, April 14, 2014

    WAWILI WAONGEZWA NGORONGORO KUTOKA STARS MPYA KUIKABILI KENYA WIKI IJAYO

    Na Mahmoud Zubeiry, Mbeya
    WACHEZAJI wawili wa nafasi za ushambuliaji, Mbwana Mshindo Mussa na Athanas Fabian Bayaga wameongezwa katika kikosi cha timu ya vijana chini ya umri wa miaka 20, Ngorongoro Heroes, ambacho kitarudiana na Kenya Aprili 27, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Afrika nchini Senegal mwakani.
    Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Ayoub Nyenzi amewatoa chipukizi hao wawili katika kambi ya timu mpya ya taifa, iliyopo Tukuyu, Mbeya kuwapeleka Dar es Salaam leo kuungana na wenzao.
    Mbwana Mshindo kulia na Athanas Bayaga kushoto wakiwa na Ayoub Nyenzi katikati Uwanja wa ndege wa Mbeya tayari kwa safari ya Dar es Salaam

    “Baada ya mechi ya kwanza na Kenya kule kwao tukitoka sare ya 0-0, mwalimu (John Simkoko) aliomba hawa vijana waongezwe, nasi kama shirikisho tumelitekeleza hilo na hivi ndiyo nawapeleka Dar es Salaam,”alisema.
    Ngorongoro imeweka kambi katika hosteli za TFF zilizopo Uwanja wa Karume, Dar es Salaa kwa ajili ya mchezo huo wa marudiano na Kenya. 
    Kikosi kinachounda timu hiyo kinajumuisha pia baadhi ya wachezaji walioonekana katika mpango wa ung’amuzi wa vipaji kwa ajili ya maboresho ya Taifa Stars.
    Wachezaji walioitwa ni makipa Aishi Manula (Azam), Hamad Juma Hamad (Scouting- Temeke), Manyika Peter Manyika (Scouting- Ilala) na Mwinyi Hassan Hamisi (Mtende, Zanzibar).
    Mabeki wa pembeni ni Ayoub Semtawa (Coastal Union), Edward Charles (JKT Ruvu), Frank Linus Makungu (Scouting- Rukwa), Gabriel Gadiel Michael (Azam), Hussein Mkongo (Ashanti United) na Ibrahim Said Mohamed (Chuoni, Zanzibar). Mabeki wa kati ni Bashiru Ismail (Tanzania Prisons), Faki Rashid Hakika (Ashanti United) na Pato Ngonyani (Majimaji).
    Viungo ni Ally Nassoro (Coastal Union), Bryson Raphael (Azam), Farid Musa (Azam), Hamid Mohamed (Mbeya City), Hassan Mbande (Mtibwa Sugar), Ibrahim Mohamed Ibrahim (Scouting- Ilala), Idd Seleman (Ashanti United), Mohamed Issa Juma (Acudu, Afrika Kusini), Muhsin Ally Muhsin (Scouting- Kinondoni), Seleman Magoma (Scouting- Ruvuma) na Tumaini John (Scouting- Mwanza).
    Washambuliaji ni Ally Salum Kabunda (Ashanti United), Ibrahim Hamad Hilika (Zimamoto, Zanzibar), Jafari Mwambusi (Mbeya City), Kelvin Friday (Azam), Ramadhan Bilal (Mlale JKT), Salum Abdilah Mineli (Ndanda) na Sibiank Lambard (Tanzania Prisons).
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: WAWILI WAONGEZWA NGORONGORO KUTOKA STARS MPYA KUIKABILI KENYA WIKI IJAYO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top