• HABARI MPYA

  Wednesday, September 18, 2013

  TANZANIA YAANZA VIBAYA MICHUANO YA AIRTEL RISING STARS

  Na Princess Asia, IMEWEKWA SEPTEMBA 18, 2013 SAA 8:14 MCHANA
  TANZANIA imeanza vibaya mashindano ya kimataifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17 ya Airtel Rising Stars baada ya jana kukubali kipigo cha mabao 2-1 kutoka kwa Ghana. Mechi ya wasichana inatarajiwa kupigwa baadae leo ambapo watakutana na Sierra-Leone.
  Mashindano ya kimataifa ya Airtel Rising Stars yanafanyika kwa mara ya pili, kwa mara ya kwanza yalifanyika nchini Nairobi na Niger kuibuka mabingwa , lengo la mashindano haya ni kuzalisha vipaji vingi vya timu za taifa barani Afrika. 
  Kikosi cha Tanzania katika michuano ya Airtel Rising Stars
  Katika mechi ya leo , Tanzania ilikua ya kwanza kupata goli katika dakika ya 26 kupitia kwa mshambuliaji hatari Athanas Mdam baada ya kuwapiga chenga mabeki wa Ghana.
  Ghana walifanya shambulizi la hatari na kupata goli la kusawazisha katika dakika ya 30 kupitia kwa Prince Agyeman baada ya kuwazidi mbio mabeki wa Tanzania na kuachia shuti kali lilimzidi mlinda mlango wa Tanzania 
  Juhudi za Tanzania kupata goli la pili hazikuzaa matunda , dakika ya 45 kipindi cha kwanza Ghana waliongeza bao la kuongoza na lililodumu mpaka kipyenga cha mwisho kupitia kwa Godfrey Nyarko baada ushirikiano mzuri wa washambuliaji wa Ghana. 
  Timu ya wavulana ambayo ipo kwenye  kundi D pamoja na Ghana , Zambia , Sierra-Leone itacheza mechi ya pili dhidi ya Zambia jumatano sembemba 18 , watamaliza na Sierra –Leone katika mchezo wa mwisho wa makundi.
  Timu ya wasichana, baada ya kucheza na Sierra –Leone  watakutana na Uganda jumatano , Septemba  18 kabla ya kukutana na Malawi siku ya Alhamisi , September 19. Mashindano yanaingia hatua ya mtoano ijumaa na fainali itapigwa jumapili , Septemba 22.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments
  Item Reviewed: TANZANIA YAANZA VIBAYA MICHUANO YA AIRTEL RISING STARS Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top