• HABARI MPYA

  Alhamisi, Septemba 19, 2013

  JAMILA ATOA ALBAMU YA TAARAB NA FILAMU KALI, SECRET OF GOD

  Na Nurat Mahmoud, IMEWEKWA SEPTEMBA 19, 2013 SAA 8: 40 MCHANA
  ALIYEWAHI kuwa mke wa wanasoka wawili maarufu nchini kwa wakati tofauti, Jamila Hassan ‘Mtoto Mzuri’ amekamilisha albamu yake ya kwanza ya muziki wa Taarab, ambayo itaingia sokoni muda si mrefu.
  Akizungumza na BIN ZUBEIRY leo, Jamila amesema kwamba albamu yake itakuwa na nyimbo nne na amemshirikisha mwimbaji maarufu wa kiume, Omar Tego.
  Mtoto Mzuri; Jamila katika pozi tofauti, ametoa albamu ya Taarab na filamu, iitwayo Secret Of God.
  Amesema kwa sasa anaweza kutaja nyimbo mbili tu ambazo ni Kimbele Front na Pole Yenu, wakati nyingine japokuwa zimekamilika, lakini hajazipa majina.
  “Mimi nimeimba nyimbo tatu na Tego ameimba wimbo mmoja. Zote hizo mbili, yangu nyingine na ya Tego bado hatujazipa majina, si unajua tena mambo ya Taarab, lazima mtu uumize kichwa,”alisema.
  Unabisha? Jamila mtoto mzuri kweli


  Jamila katika pozi la bi Harusi

  Aidha, Jamila mama wa mtoto mmoja (Nurat), amesema pia ametoa filamu inayokwenda kwa jina la Secret of God, ndani yake akicheza mwenyewe kama muhusika mkuu na pia ameshirikisha nyota wengine kadhaa.
  “Nina uzoefu wa kucheza filamu, kwa sababu kabla ya kutengeneza hii ya kwangu mwenyewe, nimewahi kucheza filamu inaitwa My Boss, filamu maarufu sana na ambayo imefanya vizuri sana,”alisema Jamila, au Mama Nurat.
  Utampenda mtoto huyu; Huyu ndiye Jamila aliyewahi kuwa mke wa wachezaji wawili tofauti nchini

  Mtoto anang'ara; Jamila huyo
  Umaarufu wa Jamila ulikuja baada ya binti huyo kuwachanganya wanasoka hao wawili kwa penzi lake- na kuvunja ndoa yake ya awali na kisha kuolewa na mchezaji mwingine. Hata hivyo, ndoa yake ya pili pia haikudumu wakatengana na sasa anaishi na mtu mwingine.
  Mama Nurat; Jamila akiwa na binti yake, Nurat

  Jamila hataki kuweka wazi kuhusu mahusiano yake mapya, lakini inadaiwa amekamata ‘kibosile wa nguvu’ ambaye anamsaidia ile mbaya katika masuala yake ya sanaa kwa sasa na ndiye huyo amezaa naye. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments
  Item Reviewed: JAMILA ATOA ALBAMU YA TAARAB NA FILAMU KALI, SECRET OF GOD Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top