IMEWEKWA SEPTEMBA 29, 2013 SAA 2:08 USIKU
KOCHA Roberto Mancini leo amekwenda mjini Istanbul, Uturukikufanya mazungumzo ya kusaini Mkataba wa miaka mitatu kuifundisha Galatasaray utakaokuwa na thamani ya Pauni Milioni 4.6 kwa mwaka.
Mancini, amekuwa 'juu ya mawe' tangu atupiwe virago Manchester City mwishoni mwa msimu na anatarajiwa kutambulishwa kurithi mikoba ya Fatih Terim Jumanne.
Mabingwa hao wa Uturuki pia wamekubali kumlipa Mtaliano huyo bonasi ya Pauni Milioni 5.86 kama watavuka hatua waliyofika mwaka jana Ligi ya Mabingwa na kufanikiwa kuingia Robo Fainali.
Kimeeleweka: Roberto Mancini yupo Uturuki kukamilisha mazungumzo ya kujiunga na Galatasary
Juu ya mawe noma: Mancini alifukuzwa Manchester City Mei, mwaka huu
Mancini anatarajiwa kukutana na Rais wa klabu, Unal Aysal Jumatatu kufikia makubaliano ya mwisho ya Mkataba, kwa mujibu wa wakala Muzzi Ozcan ambaye alifanikisha kuziunganisha pande hizo mbili, baada ya klabu hiyo kumfukuza Terim.
Uturuki sasa: Galatasaray inamtaka Mtaliano huyu