• HABARI MPYA

  Alhamisi, Septemba 26, 2013

  NI ARSENAL NA CHELSEA RAUNDI YA NNE KOMBE LA LIGI, UNITED NA VIBONDE NORWICH, NEWCASTLE NA MAN CITY

  IMEWEKWA SEPTEMBA 26, 2013 SAA 7:40 USIKU
  KLABU ya Arsenal itamenyana na wapinzani wao katika Jiji la London, Chelsea katika Raundi ya Nne ya Kombe la Ligi, maarufu kama Capital One Cup baada ya kuitoa West Brom kwa penalti 4-3 Uwanja wa Hawthorns.
  Mechi hiyo imeisha kwa sare ya 1-1 usiku huu, lakini penalti walizokosa Morgan Amalfitano na Craig Dawson zinawasongesha mbele Gunners.
  Through: United progressed on Wednesday night with a 1-0 win over Liverpool at Old Trafford
  Mbele: United imesonga mbele kwa ushindi wa 1-0 dhidi ya Liverpool Uwanja wa Old Trafford

  RATIBA KAMILI RAUNDI YA NNE CAPITAL ONE

  Sunderland v Southampton
  Leicester City v Fulham
  Birmingham City v Stoke City
  Manchester United v Norwich City
  Burnley v West Ham United
  Arsenal v Chelsea
  Tottenham v Hull City
  Newcastle v Manchester City
  Mechi zote zitachezwa Jumanne ya Oktoba 29 na Jumatano ya Oktoba 30.
  Manchester United baada ya kuwatoa wapinzan wao, Liverpool watamenyana na Norwich nyumbani katika Raundi ya Nne.
  Bao pekee la Javier Hernandez mapema kipindi cha pili katika ushindi wa 1-0 Old Trafford, linawakutanisha Mashetani Wekundu na The Canaries Oktoba 28.
  Birmingham iliyowatoa mabingwa watetezi Swansea kwa mabao 3-1 watacheza tena nyumbani katika 16 Bora, safari hii wakimenyana na timu ya Mark Hughes, Stoke.
  Licha ya kupangiwa wapinzani wagumu, lakini The Blues bado wanapewa nafasi kubwa ya kutwaa tena taji walilolitwaa mwaka 2011, na United ikiwa timu nyingine inayopewa nafasi pia baada ya kupangiwa Norwich.
  Katika mechi nyingine, Newcastle itaikaribisha Manchester City Uwanja wa St James Park baada ya kuwatoa Leeds, wakati Hull wataifuata Tottenham siku kadhaa baada ya kucheza mechi ya Ligi Kuu, Uwanja wa White Hart Lane.
  Timu isiyo na kocha kwa sasa, Sunderland itamenyana na Southampton, wakati West Ham watakwedna Kaskazini kumenyana na Burnley.
  Fulham ya Martin Jol itaifuata Leicester kusaka nafasi ya Robo Fainali.

  MIKWAJU YA PENALTI

  West Brom: Reid (penalti ya kwanza) amefunga, Rosenberg amefunga, Morrison amefunga, Dawson amekosa, Amalfitano amekosa
  Arsenal: Bendtner amefunga, Gnabry amekosa, Olsson amefunga, Akpom amefunga, Monreal amefunga
  Arsenal imeifunga West Brom kwa penalti 4-3
  Arsenal iliendeleza wimbi la ushindi kwa kuitoa kwa matuta West Brom Uwanja wa The Hawthorns na kuingia Raundi ya Nne.
  Eisfeld aliifungia Arsenal dakika ya 61 kabla ya Berahino kusawazisha dakika ya 71.
  Kikosi cha West Brom kilikuwa: Daniels, Reid, Popov, Lugano, Dawson, Sinclair, Dorrans, Mulumbu/Morrison dk91, Berahino/Amalfitano dk101, Long/Rosenberg dk91, Sessegnon
  Arsenal: Fabianski, Mertesacker, Vermaelen, Monreal, Jenkinson, Arteta/Bellerin dk95, Miyaichi, Gnabry, Hayden/Kris Olsson dk84, Bendtner, Eisfeld/Akpom dk82.
  Keeping his cool: Nacho Monreal stepped up to convert the winning penalty for Arsenal
  Ya ushindi: Nacho Monreal akiifungia Arsenal penalti ya ushindi
  Cue celebrations: Monreal's Arsenal team-mates rushed to congratulate the Spaniard after his strike
  Shangwe: Monreal na wachezaji wenzake wa Arsenalwakishangilia
  Nice work: Arsene Wenger talks to the returning Nicklas Bendtner before his penalty
  Kazi nzuri: Arsene Wenger akizungumza na Nicklas Bendtner kabla ya kupiga penalti yake
  Cool: Arsenal's Thomas Eisfeld netted the opener for the visitors after the hour mark
  Thomas Eisfeld akiifungia bao la kwanza Arsenal
  Neat finish: Thomas Eisfeld wheels away, celebrating his first senior goal for Arsenal
  Thomas Eisfeld akiondoka kushangilia bao lake
  Incoming: Nicklas Bendtner collides with the post in the first half at The Hawthorns
  Amerejea: Nicklas Bendtner alikuwa mwiba usiku huu The Hawthorns
  Incoming: Nicklas Bendtner collides with the post in the first half at The Hawthorns
  Incoming: Nicklas Bendtner collides with the post in the first half at The Hawthorns
  New look: The Denmark striker donned a beard and a David Beckham-esque haircut
  Mwonekano mpya: Mdenmark amekuja kwa staili ya nywele za David Beckham
  Congratulations: Bendtner and Eisfeld are mobbed by team-mates after Arsenal opened the scoring
  Pongezi: Bendtner na Eisfeld wakipongezwa na wachezaji wenzao
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments
  Item Reviewed: NI ARSENAL NA CHELSEA RAUNDI YA NNE KOMBE LA LIGI, UNITED NA VIBONDE NORWICH, NEWCASTLE NA MAN CITY Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top