• HABARI MPYA

  Wednesday, September 25, 2013

  RHINO RANGERS YAISHUSHA YANGA LIGI KUU BAADA YA KUICHAPA ASHANTI UNITED LEO TABORA

  Na Nurat Mahmoud, IMEWEKWA SEPTEMBA 25, 2013 SAA 3:53 USIKU
  RHINO Rangers imepata ushindi wa kwanza katika Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara msimu huu, baada ya leo kuilaza Ashanti United mabao 2-0 Uwanja wa Ally Hassan Mwinyi, Tabora.
  Kwa ushindi huo, timu hiyo ya Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) imefikisha pointi saba na kupanda hadi nafasi ya nane ikiwashusha kwa nafasi moja, mabingwa watetezi, Yanga SC.
  Juu ya mabingwa; Rhino leo wameishusha Yanga kwa nafasi moja 

  Katika mchezo huo, mabao ya Rhino yalifungwa na Kamana Salum dakika ya 26 na Hussein Abdallah dakika ya 64.
  Ligi hiyo itaendelea Jumamosi wakati, Yanga SC itakapomenyana na Ruvu Shootings Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na Rhino Rangers wakiikaribisha Ashanti United Mwinyi, Tabora.
  Mechi nyingine zitapigwa Jumapili, Simba SC ikishuka dimbani Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kumenyana na JKT Ruvu, Rhino Rangers na Kagera Sugar Uwanja wa Ally Hassan Mwinyi, Tabora, Mbeya City na Coastal Union Sokoine, Mbeya, Mgambo JKT na JKT Oljoro Mkwakwani, Tanga na Ashanti United na Mtibwa Sugar, Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments
  Item Reviewed: RHINO RANGERS YAISHUSHA YANGA LIGI KUU BAADA YA KUICHAPA ASHANTI UNITED LEO TABORA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top