• HABARI MPYA

    Monday, September 30, 2013

    MCHAKATO WA KATIBA MPYA SIMBA SC WAINGIA AWAMU YA PILI

    Na Ezekiel Kamwaga, IMEWEKWA SEPTEMBA 30, 2013 SAA 10:12 JIONI
    MARA baada ya kupokea maoni mbalimbali kutoka kwa wadau wake kuhusu mapendekezo ya Katiba mpya, klabu ya Simba sasa inaingia katika awamu ya pili ya mchakato huo, ambayo ni kupokea maoni ya Matawi yake. 
    Taarifa ya Simba SC leo imesem kwamba baada ya kumalizika kwa hatua hiyo ya kwanza, matawi ya Simba sasa yanakaribishwa kuanza kutoa maoni yao kuanzia kesho.
    Matawi yatajadili na kutoa maoni yao kabla ya kuwasilisha kwa sekretarieti ya klabu iliyopo katika Ofisi za Makao Makuu Mtaa wa Msimbazi Dar es Salaam na Sekretarieti ya Simba itayapokea maoni haya hadi Oktoba 11 mwaka huu.
    Leteni maoni ya Katiba mpya; Mwenyekiti wa Simba SC, Alhaj Ismail Aden Rage

    “Sekretarieti ya klabu itayakusanya na kuyachambua maoni yote yaliyotolewa na baada ya uchambuzi huo, yatapelekwa kwa wajumbe wa Kamati ya Utendaji ya Klabu ambao nao watafanya mapitio yao,”.
    “Uchambuzi na mapitio yatakayofanywa kwa baraka za Kamati ya Utendaji ndiyo ambayo yatapelekwa kwenye kikao cha Matawi kilichopangwa kufanyika Novemba 11 mwaka huu,”.
    “Wiki moja baadaye, yaani Novemba 19 mwaka huu, Kamati ya Utendaji kwa ridhaa iliyopewa na Katiba ya Simba SC, itapitisha vipengele vya kuombewa mabadiliko ya Katiba,”.
    “Vipengele hivyo ndivyo ambavyo vitawasilishwa Novemba 24 mwaka huu kwenye Mkutano Maalumu wa Mabadiliko ya Katiba uliotangazwa kufanyika na klabu katika Mkutano Mkuu wa wanachama uliopita,”.
    “Uongozi unawaomba wanachama kupitia matawi yao kushiriki kikamilifu katika mchakato huu adhimu kwa klabu. Ni matarajio ya klabu kwamba mchakato huu hautatumika kuwagawa bali kuwafanya wawe kitu kimoja kwa faida ya Simba,”.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: MCHAKATO WA KATIBA MPYA SIMBA SC WAINGIA AWAMU YA PILI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top