• HABARI MPYA

  Saturday, September 21, 2013

  UMONY, MIENO NA BOCCO FITI KUIVAA YANGA SC TAIFA...JANGWANI KAZI WANAYO KESHO

  Na Prince Akbar, IMEWEKWA SEPTEMBA 21, 2013 SAA 4:44 ASUBUHI
  HABARI njema kwa wapenzi wa Azam FC kuelekea mchezo wa kesho wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya Yanga SC ni kwamba wachezaji wote tegemeo waliokuwa majeruhi sasa wako fiti kwa asilimia 100.
  Kiungo Mkenya, Humphrey Mieno na washambuliaji, Mganda Brian Umony na mzawa, John Bocco wote wako fiti kwa ajili ya mchezo wa kesho.
  Meneja wa Azam FC, Jemadari Said Kazumari amesema majeruhi pekee ambaye hajarejea kazini ni Samih Hajji Nuhu ambaye yuko India kwa matibabu.
  Kuelekea mchezo huo wa kesho, Jemadari amesema kikosi kipo imara kabisa na maandalizi yamekamilka, kilichobaki ni kuwafunga Yanga SC kesho Taifa.
  Brian Umony amerudi uwanjani na ataivaa Yanga SC kesho

  Azam imefungwa mechi nne mfululizo na Yanga SC tangu Fainali ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame msimu uliopita, yaani pamoja na mechi mbili za Ligi Kuu msimu uliopita na mchezo wa Ngao ya Jamii msimu huu. 
  Lakini kurejea kwa nyota wake hao waliokuwa nje kwa muda mrefu kunaleta matumaini kwa kocha wa Azam, Muingereza Stewart Hall kufuta uteja kwa Yanga SC inayofundishwa na Mholanzi, Ernie Brandts kesho.
  Yanga na Azam zinalingana kwa pointi, sita kila timu baada ya kucheza mechi nne msimu huu, maana yake zinazidiwa pointi nne na vinara wa Ligi Kuu, Simba SC wenye pointi 10 kileleni. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments
  Item Reviewed: UMONY, MIENO NA BOCCO FITI KUIVAA YANGA SC TAIFA...JANGWANI KAZI WANAYO KESHO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top