• HABARI MPYA

  Sunday, September 29, 2013

  SUAREZ AFUNGA MARA MBILI LIVERPOOL IKIIKUNG'UTA SUNDERLAND 3-1 LIGI KUU ENGLAND

  IMEWEKWA SEPTEMBA 29, 2013 SAA 3:50 USIKU
  MSHAMBULIAJI Luis Suarez amerejea na moto katika Ligi Kuu ya England baada ya kumaliza adhabu yake ya mechi 10, leo akifunga mabao mawili katika ushindi wa 3-1 wa Liverpool dhidi ya Sunderland.
  Ntyota huyo wa Uruguay alifunga mabao yake katika dakika za 36 na 89 wakati lingine lilifungwa na mshambuliaji pacha wake, Daniel Sturridge dakika ya 28 na kufutia machozi la wenyeji lifungwa na Emanuele Giaccherini dakika ya 52.
  BADGES
  Kikosi cha Liverpool kilikuwa: Mignolet, Toure, Skrtel, Sakho, Henderson, Gerrard, Lucas, Jose Enrique, Moses/Sterling dk75, Sturridge na Suarez.
  Sunderland: Westwood, Gardner, O'Shea, Cuellar, Colback, Larsson/Mavrias dk85, Cattermole/Celustka dk74, Ki,Johnson, Altidore na Giaccherini.
  Family guy: Luis Suarez celebrates by showing a picture of his wife and daughter with new son Benjamin
  Baba wa familia: Luis Suarez akishangilia kwa kuonyesha picha ya mkewe na binti yake na mtoto wake mpya wa kiume, Benjamin
  Back with a bang: Suarez scores his first goal since his ban
  Amerudi na moto: Suarez amefunga kwa mara ya kwanza baada ya kumaliza adhabu
  Sliding in: Suarez scores his side's second goal at the back post
  Suarez akiifungia timu yake bao la pili
  They all count: Daniel Sturridge opened the scoring with a scrappy goal
  Daniel Sturridge alifunga bao la kwanza
  Opening up: Sturridge celebrates scoring Liverpool's first goal
  Sturridge akishangilia baada ya kufunga bao la kwanza
  In good form: Sturridge celebrates his seventh goal of the season
  Sturridge akishangilia bao lake la saba msimu huu
  Tangled up: Victor Moses and Jack Colback compete for the ball
  Victor Moses akigombea mpura na Jack Colback
  Stop there: Martin Skrtel tackles Sunderland's Jozy Altidore
  Martin Skrtel akimaa miguuni Jozy Altidore
  Heads up: Altidore is challenged by Kolo Toure
  Altidore akipambana na Kolo Toure
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments
  Item Reviewed: SUAREZ AFUNGA MARA MBILI LIVERPOOL IKIIKUNG'UTA SUNDERLAND 3-1 LIGI KUU ENGLAND Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top