• HABARI MPYA

  Ijumaa, Septemba 27, 2013

  MMILIKI ARSENAL ASEMA WENGER ANABAKI ARSENAL...NA ANAPEDNA ABAKI KWA MUDA MREFU SANA TU EMIRATES

  IMEWEKWA SEPTEMBA 27, 2013 SAA 3:00 ASUBUHI
  CHIFU wa Arsenal, Stan Kroenke anataka kocha Arsene Wenger abaki katika klabu hiyo kwa muda mrefu na kuleta taji la Ligi Kuu ya Enland Emirates.
  Mfaransa huyo amekuwa katika klabu hiyo kwa miaka 17 na The Gunners ikiwa inakabiliwa na ukame wa mataji kwa msimu wa tisa sasa, amekuwa akipigwa zengwe aondoke, hususan kutokana na Mkataba wake kumalizika mwishoni mwa msimu.
  Lakini mtu mwenye hisa nyingi za klabu, Kroenke hana shaka anataka Wenger abaki.
  Form: Wenger endured a tough summer, but his side have the momentum early on in the season
  Atabaki: Mkataba wa Wenger unamalizika mwishoni mwa msimu, lakini anaweza kubaki
  Support: Kroenke is fully behind Wenger, and believes Suarez was never going anywhere
  Anayemkingia kifua: Kroenke anamkingia kifua Wenger, na aanamini Suarez asingeondoka

  Mmarekani huyo amesema kwamba hafikiri kama kuna mwingine bora kuliko yeye na anaamini Wenger anafanya kazi nzuri.
  Alipoulizwa kama mwalimu huyo mwenye umri wa miaka 63 yumo kwenye mipango ya muda mrefu ya klabu hiyo, Kroenke alisema: "Hiyo ni sahihi kabisa. Arsene anafahamu ambavyo tunahisi, falsafa zetu ni nini, nini tunataka kufanya na ninahisi tuko pamoja sana,".
  Kufuatia klabu kuvuna rekodi yake ya usajili kwa kumsaini Mesut Ozil kutoka Real Madrid, Kroenke ameweka wazi kwamba fedha zitaendelea kutolewa kwa ajili ya kuimarisha kikosi.
  Finally: Luis Suarez was back in action for Liverpool as his side took on Manchester United
  Hatimaye: Luis Suarez alirejea kazini Liverpool timu yake ikimenyana na Manchester United

  Kroenke alisema: "Kwa kweli namfurahia Arsene - safi sana, mweledi. Ana upeo mkubwa wa uongoza timu na klabu. Yuko sahihi katika hilio.
  Kroenke pia amesema Wenger hastahili lawama kwa klabu hiyo la Kaskazin mwa London kumkosa mshambuliaji Luis Suarez, kwani ni Liverpool ndio hawakuwa tayari kumuuza nyota huyo wa Uruguay.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments
  Item Reviewed: MMILIKI ARSENAL ASEMA WENGER ANABAKI ARSENAL...NA ANAPEDNA ABAKI KWA MUDA MREFU SANA TU EMIRATES Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top