• HABARI MPYA

    Saturday, September 21, 2013

    CHELSEA YAUA 2-0...OBI MIKEL AFUNGA BAO LA KWANZA LIGI KUU ENGLAND, MOURINHO AENDELEZA REKODI YA KUTOFUNGWA NDANI YA MECHI 63 DARAJANI

    IMEWEKWA SEPTEMBA 21, 2013 SAA 3:59 USIKU
    KIUNGO John Obi Mikel amefunga bao lake la kwanza katika Ligi Kuu ya England na kuiwezesha Chelsea kuibuka na ushindi wa 2-0 dhidi ya Fulham Uwanja wa Stamford Bridge, huo ukiwa ushindi wao wa kwanza mwezi huu.
    Mabao ya Oscar na Mikel kipindi cha pili yamemaliza ukame wa ushindi ndani ya mechi nne na kuendeleza rekodi ya Jose Mourinho kutofungwa nyumbani katika Ligi Kuu ndani ya mechi 63 na ushndi wa kwanza tangu wafungwe na Aston Villa.
    Ushindi huo wa 2-0 unamaanisha Fulham inatimiza miaka 34 bila kushinda Stamford Bridge, Chelsea ikizinduka baada ya vipigo vya Everton na Basle.
    Kikosi cha Chelsea kilikuwa: Cech, Ivanovic, Cahill, Terry, Cole, Ramires, Mikel, Schurrle/Lampard dk79, Oscar, Hazard/De Bruyne dk85, Eto’o/Torres dk64.
    Fulham: Stockdale, Riether, Amorebieta, Hangeland, Richardson, Duff/Taarabt dk64, Parker, Sidwell, Kacaniklic/Tue Na Bangna dk72, Kasami/Rodallega dk85 na Bent.
    Back to winning ways: Oscar celebrates his goal - Chelsea's first in more than four hours of Premier League football
    Ushindi umerudi: Oscar akishangilia bao lake na wenzake
    On target: Oscar breaks the deadlock at Stamford Bridge
    Oscar amefunga bao la kwanza leo Stamford Bridge
    A rarity: John Obi Mikel stretches to score his first goal for 258 matches
    Bao tamu sana: John Obi Mikel akifunga bao lake la kwanza Ligi Kuu England baada ya mechi 258
    Ecstatic: The midfielder was delighted with his goal
    Raha sana: Obi akishangilia bao lake
    Back to winning ways: Jose Mourinho celebrated his first win in a month
    Raha zimerejea Darajani: Jose Mourinho akishangilia ushindi wake wa kwanza mwezi huu
    Slightly better: Roman Abramovich was in the stands again to watch the victory
    Mwenye timu tabasamu latosha: Roman Abramovich akiwa jukwaani kuangalia ushindi wa timu yake
    Golden: Darren Bent missed a brilliant chance when the game was still 0-0
    Amekosa: Darren Bent alipoteza nafasi nzuri ya kufunga wakati timu hizo hazijafungana
    In pain: Scott Parker is felled by Gary Cahill
    Maumivu: Scott Parker akichezewa rafu na Gary Cahill
    Flattened: Steve Sidwell leaves Eden Hazard on the floor after a challenge
    Hdi chini: Steve Sidwell akimuacha chini Eden Hazard baada ya kugombea naye mpira
    Drawing a blank: Samuel Eto'o again failed to find the mark for his new club
    Mabao wapi?: Samuel Eto'o kwa mara nyingine ameshindwa kuifungia timu yake mpya
    Up in the air: John Terry directs the ball towards goal from a corner
    John Terry akiwania mpira wa juu
    Under pressure: Branislav Ivanovic is closed down by Pajtim Kasami
    Branislav Ivanovic akipambana na Pajtim Kasami
    Battle: Ramires, attempts to tackle Alexander Kacaniklic
    Ramires, akipambana na Alexander Kacaniklic
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: CHELSEA YAUA 2-0...OBI MIKEL AFUNGA BAO LA KWANZA LIGI KUU ENGLAND, MOURINHO AENDELEZA REKODI YA KUTOFUNGWA NDANI YA MECHI 63 DARAJANI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top