• HABARI MPYA

  Jumamosi, Septemba 21, 2013

  LIVERPOOL YAPIGWA KIDUDE NYUMBANI, SUAREZ AKIMALIZA ADHABU YA MECHI 10

  IMEWEKWA SEPTEMBA 21, 2013 SAA 3:24 USIKU
  BAO pekee la Dejan Lovren limeipa Southampton ushindi wa 1-0 Uwanja wa Anfield dhidi ya wenyeji Liverpool leo.
  Mwanasoka huyo wa kimataifa wa Croatia alifunga bao hilo dakika ya 54 na kumaliza rekodi ya Liverpool kutofungwa ndani ya mechi 12.
  Mshambuliaji Luis Suarez, alikuwepo jukwaani akishuhudia mechi yake hiyo ya mwisho katika adhabu ya kufungiwa mechi 10 na sasa anarejea uwanjani.
  Pamoja na hayo The Saints, inabidi wamshukuru refa Neil Swarbrick aliyewanyima Liverpool penalti baada ya beki wao kumuangusha Daniel Sturridge kwenye eneo la hari kipindi cha kwanza.
  Kikosi cha Liverpool kilikuwa: Mignolet, Toure, Skrtel/Alberto dk72, Agger/Enrique dk56, Sakho, Gerrard, Lucas, Henderson, Aspas/Sterling dk46, Moses na Sturridge.
  Southampton: Boruc, Clyne, Lovren/Fonte, Shaw, Wanyama, Schneiderlin, Rodriguez/Cork dk89, Lallana/Ward-Prowse dk75, Osvaldo, Lambert/Davis dk61.
  Brilliant win: Dejan Lovren scored the only goal of the game as Southampton ended Liverpool's unbeaten start to the season
  Bao la ushindi: Dejan Lovren amfunga bao pekee la ushindi dhidi ya LiverpoolOn target: Saints players cheer as Lovren's header hits the back of the net
  Amepatia: Wachezaji wa Liverpool wakiangalia mpira uliopigwa kwa kichwa na Lovren ukitinga nyavuniGreat scenes: Lovren takes the plaudits from the Southampton fans
  Babu kubwa: Lovren akishangilia mbele ya mashabiki wa SouthamptonOff target: Daniel Sturridge show his anguish after missing a chance
  Amekosa: Daniel Sturridge aisikitika baada ya kupoteza nafasi ya kufunga
  Brendan Rogers
  Steven Gerrard
  Hasira: Brendan Rodgers na Steven Gerrard wakionyesha hasira zao za kufungwaHome debut: Victor Moses made his first appearance at Anfield in red
  Kifaa: Victor Moses akiichezea Liverpool kwa mara ya kwanza Uwanja wa AnfieldTussle: Kolo Toure and James Rodriguez battle for possession
  Jino kwa jino: Kolo Toure na James Rodriguez wakigombea mpiraStrike: Steven Gerrard hits a free kick
  Mkwaju: Steven Gerrard akipiga mpira wa adhabuBattle: Mamadou Sakho and Nathaniel Clyne vie for the ball
  Vita: Mamadou Sakho na Nathaniel Clyne wakigombea mpiraWatching on: Luis Suarez watches the action at Anfield
  Anatazama: Luis Suarez akiangalia mechi AnfieldChallenge: Adam Lallana rides a tackle from Steven Gerrard
  Mchuano: Adam Lallana akipambana na Steven Gerrard
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments
  Item Reviewed: LIVERPOOL YAPIGWA KIDUDE NYUMBANI, SUAREZ AKIMALIZA ADHABU YA MECHI 10 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top