• HABARI MPYA

    Thursday, September 19, 2013

    MESSI AJIBU HAT TRICK YA RONALDO, BARCA IKIITANDIKA 4-0 AJAX, MUNTARI AIFUNGIA AC MILAN IKIICHAPA CELTIC 2-0

    IMEWEKWA SEPTEMBA 19, 2013 SAA 7:14 USIKU
    AMEJIBU; Lionel Messi amejibu mapigo ya mpinzani wake, Cristiano Ronaldo wa Real Madrid baada ya kuifungia hat-trick Barcelona katika ushindi wa 4-0 dhidi ya Ajax katika mchezo wa Kundi H Ligi ya Mabingwa Ulaya, Uwanja wa Nou Camp.
    Muargentina huyo pamoja na kufunga mabao matatu peke yake usiku, pia alitengeneza bao la nne lililofungwa na Gerard Pique.
    Haikuwa bahati yao, Ajax kwani walikosa hadi penalti baada ya kipa Victor Valdes kuokoa mkwaju wa Kolbeinn Sigthorsson.
    Messi alifunga mabao yake katika dakika za 22, 55 na 75, wakati Pique alifunga dakika ya 69.
    Kikosi cha Barcelona kilikuwa: Valdes, Alves, Pique/Bartra dk80, Mascherano, Adriano, Busquets, Fabregas/Xavi dk72, Iniesta, Sanchez, Messi, Neymar /Pedro dk72.
    Ajax: Vermeer, van Rhijn, Denswil, Moisander/van der Hoorn dk73, Blind/Schone dk78, Poulsen, de Jong/Serero dk59, Duarte, Bojan, Sigthorsson na Boilesen.
    Precision: Messi bends in a long-range free-kick for his first goal of the evening
    Mkwaju: Messi alifunga bao la kwanza kwa shuti la mbali la mpira wa adhabu
    Number two: Messi slots his second goal past the helpless Vermeer
    La pili: Messi akifunga bao lake la pili
    Easy: Messi dribbles past defender Stefano Denswil
    Kiulaini: Messi akimtoka beki Stefano Denswil
    All smiles: Messi celebrates his opener with defener Dani Alves
    Tabasamu: Messi akishangilia na beki wake, Dani Alves
    Battle: Sergio Busquets shields the ball from Ajax's Siem de Jong (left) and Lerin Duarte
    Sergio Busquets akidhibiti mpira katikati ya wachezaji wa Ajax, Siem de Jong (kushoto) na Lerin Duarte
    Wasted opportunity: Kolbeinn Sigthorsson takes an unsuccessful penalty against Victor Valdes
    Anakosa: Kolbeinn Sigthorsson alikosa penalti iliyochezwa na kipa Victor Valdes
    Challenge: Alexis Sanchez tackles Ajax's Daley Blind at the Camp Nou
    Alexis Sanchez akimvaa Daley Blind wa Ajax Uwanja wa the Camp Nou
    Tussle: Barcelona defender Adriano attempts to block Ajax's Ricardo van Rhijn
    Beki wa Barcelona, Adriano akimdhibiti Ricardo van Rhijn wa Ajax
    Heads up: Pique rises highest to score Barcelona's third goal
    Pique akienda hewani kuifungia Barcelona bao la tatu
    Frustration: Neymar grimaces after missing an opportunity to score
    Hasira: Neymar aking'aka baada ya kupoteza nafasi ya kufunga
    Old friends: Javier Mascherano challenges loanee Bojan Krkic for the ball
    Marafiki wa zamani: Javier Mascherano akichuana na Bojan Krkic anayecheza kwa mkopo
    On form: Barca celebrate three points at the Camp Nou
    Wako vizuri: Barca wakishangilia ushindi wao Camp Nou

    Katika mchezo mwingine wa kundi hilo, AC Milan iliichapa Celtic 2-0 Uwanja wa San Siro, mabao ya Zapata dakika ya 82 na Muntari dakika ya 85.
    Kikosi cha AC Milan kilikuwa: Abbiati, Zaccardo, Zapata, Mexes, Constant/Robinho dk76, Nocerino, De Jong, Muntari, Birsa/Emanuelson dk64, Matri/Poli dk87 na Balotelli.
    Celtic: Forster, Lustig, Van Dijk, Ambrose, Izaguirre, Matthews/Boerrigter dk75, Brown, Mulgrew/Biton dk89, Samaras, Commons/Pukki dk77 na Stokes.Christian Zapata
    Christian Zapata akitimka kushangilia baada ya kuifungia bao la kwanza AC Milan dhidi ya Celtic
    Sulley Muntari
    Mwafrika hatari: Sulley Muntari wa Milan akishangilia baada ya kufunga bao la pili zikiwa zimebaki dakika tano
    Cristian Zapata
    Phillipe Mexes akimrukia Cristian Zapata baada ya Mcolombia kufunga
    Charlie Mulgrew
    Ukuta mgumu: Wachezaji wa AC Milan wakiwa wameweka ukutawakati beki wa kati wa Celtic, Charlie Mulgrew akipiga mpira wa adhabu
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: MESSI AJIBU HAT TRICK YA RONALDO, BARCA IKIITANDIKA 4-0 AJAX, MUNTARI AIFUNGIA AC MILAN IKIICHAPA CELTIC 2-0 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top