• HABARI MPYA

  Ijumaa, Septemba 20, 2013

  SWANSEA YAICHAPA 3-0 NYUMBANI KWAKE VALENCIA EUROPA LEAGUE, SPURS NAYO YAUA 3-0 NYUMBANI

  IMEWEKWA SEPTEMBA 20, 2013 SAA 6:11 USIKU
  WAKALI wa soka ya kitabuni England, Swansea wameanza vyema Europa League baada ya kuifumua mabao 3-0 nyumbani kwake Valencia iliyomaliza na wachezaji 10.
  Wenyeji walilazimika kucheza 10 kwa takriban dakika 80, baada ya beki Adil Rami kutolewa nje kwa kadi nyekundu, kufuatia kumchezea rafu Wilfried Bony.
  Mshambuliaji huyo ndiye aliyeifungia Swansea bao la kwanza dakika ya 14 usiku huu, hilo likiwa bao lake la tano katika mechi nanemsimu huu.
  Mabao mengine yalifungwa na Michu dakika ya 58 na Jonathan de Guzman dakika ya 62.
  Kikosi cha Valencia kilikuwa: Guaita, Barragan, Rami, Feghouli/Pabon dk59, Mathieu, Ever/Costa dk14, Javi Fuego, Guardado, Canales/Bernat dk66, Cartabia na Postiga. 
  Swansea: Vorm, Rangel/Davies dk56, Amat, Chico, Tiendalli, de Guzman, Canas, Pozuelo, Dyer/Lamah dk65, Michu/Shelvey dk77 na Bony. 
  Bang: Wilfried Bony scores the first at Valencia
  Kitu hicho: Wilfried Bony akiifungia bao la kwanza Swansea dhidi ya Valencia
  Helping hand: Swansea were aided early on when Adil Rami was sent off
  Nenda Nje: Adil Rami akionyeshwa kadi nyekundu
  Up and running: Swansea celebrate after Wilfried Bony scored the club's first European goal
  Pati la ushindi: Swansea wakishangilia baada ya Wilfried Bony kufunga

  Katika mchezo mwingine, mabao mawili ya Jermain Defoe yalichgia ushindi wa 3-0 kwa Tottenham dhidi ya Tromso, bao lingine akifunga Christian Eriksen .
  Pamoja na ushindi huo, Mousa Dembele, Danny Rose and Younes Kaboul wote walitoewa nje baada ya kuumia.
  Tottenham ilimaliza mechi na wachezaji 10 kutokana na Kaboul kutolewa nje baada ya kuumia, wakati kocha Andre Villas-Boas amemaliza idadi ya wachezaji wa kubadili.
  Spurs: Lloris, Naughton, Kaboul, Dawson, Rose, Sandro, Dembele, Sigurdsson, Holtby, Lamela na Defoe.
  Tromso: Sahlman, Kristiansen, Fojut, Koppinen, Causevic, Bendiksen, Johansen, Drage, Pritchard, Moldskred, Ondrasek.
  Goal king: Jermain Defoe scored twice in the first half as Spurs cruised to victory
  Mfalme wa mabao: Jermain Defoe ameifungia mabao mawili Spurs
  Cool finish: Defoe puts his shotpast Tromso's goalkeeper Marcus Sahlman for the opening goal
  Safi hiyo: Defoe akimtungua kipa wa Tromso, Marcus Sahlman kufunga la kwanza
  Closing down: Michael Dawson vies for the ball with Tromso's Josh Pritchard
  Michael Dawson akigombea mpira na Josh Pritchard wa Tromso
  Two easy: Defoe scores his and Tottenham's second goal of the goal
  La pili kiulaini: Defoe akifunga bao tamu
  Jump to it: Defoe celebrates scoring his second goal with Lewis Holtby
  Ruka juu: Defoe akishangilia na Lewis Holtby baada ya kufunga
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments
  Item Reviewed: SWANSEA YAICHAPA 3-0 NYUMBANI KWAKE VALENCIA EUROPA LEAGUE, SPURS NAYO YAUA 3-0 NYUMBANI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top