• HABARI MPYA

  Sunday, September 29, 2013

  SIMBA SC ILIYOZIDI KUPAA LIGI KUU LEO, ANGALIA MAVITU YA TAMBWE SI MCHEZO

  IMEWEKWA SEPTEMBA 29, 2013 SAA 3:24 USIKU
  Mshambuliaji wa Simba SC, Amisi Tambwe akipambana na beki wa JKT Ruvu, Omar Mtaki anayecheza kwa mkopo kutoka Azam FC, katika mchezo wa leo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Simba SC ilishinda 2-0.

  Kiungo wa Simba SC, Abdulhalim Humud 'Gaucho' akienda chini baada ya kuchezewa rafu na beki wa JKT Ruvu, Amos Mgisa

  Mshambuliaji wa Simba SC, Betram Mombeki akibusu kiatu cha kiungo Ramadhani Singano 'Messi' baada ya kufunga bao la pili 

  Abdulhalim Humud akimtoka Salum Machaku kabla ya kupiga krosi iliyozaa bao la pili 

  Haroun Chanongo akipambana na beki wa JKT Ruvu

  Amos Mgisa akituliza mpira gambani mbele ya beki wa Simba SC, Adeyoum Seif

  Gilbert Kaze wa Simba SC kushoto akigombea mpira na Bakari Kondo wa JKT Ruvu

  Haruna Shamte wa Simba SC akipambana na mchezaji wa JKT Ruvu

  Bakari Kondo akimtoka Gilbert Kaze wa Simba SC 

  Alhaj Zege wa JKT Ruvu akipambana na Adeyoum Seif wa Simba SC kulia

  Omar Mtaki wa JKT Ruvu anayecheza kwa mkopo kutoka Azam, akimdhibiti Betram Mombeki

  Abdulhalim Humud 'Gaucho' akimuacha chini Salum Machaku

  Amri Kiemba akimtoka Salum Machaku

  Amri Kiemba akimuacha chini Nashon Naftali wa JKT Ruvu

  Omar Mtaki alimdhibiti vizuri Amisi Tambwe akaambulia kufunga bao moja tu kwa penalti

  Mtaisoma SImba 2013; Mashabiki wa Simba SC kwa raha zao

  Haloo, Simba SC mwaka huu inatisha; Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba SC, Zacharia Hans Poppe kushoto akizungumza na simu huku akifuatilia mchezo 

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments
  Item Reviewed: SIMBA SC ILIYOZIDI KUPAA LIGI KUU LEO, ANGALIA MAVITU YA TAMBWE SI MCHEZO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top