• HABARI MPYA

  Sunday, September 22, 2013

  SIMBA, MBEYA CITY ZAINGIZA MILIONI 123

  Na Boniface Wambura, IMEWEKWA SEPTEMBA 22, 2013 SAA 3:38 ALASIRI
  MECHI ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) kati ya Simba na Mbeya City iliyochezwa jana (Septemba 21 mwaka huu) kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam imeingiza sh. 123,971,000.
  Watazamaji 21,936 ndiyo waliokata tiketi kushuhudia mechi hiyo namba 32 ya VPL msimu wa 2013/2014 iliyomalizika kwa timu hizo kutoka sare ya mabao 2-2.
  Viingilio katika mechi hiyo vilikuwa sh. 5,000, sh. 8,000, sh. 15,000 na sh. 20,000 huku kila klabu ikipata mgawo wa sh. 30,064,741.95 wakati Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) iliyolipwa ni sh. 18,910,830.51.
  Betram Mombeki wa Simba SC akiwatoka mabeki wa Mbeya City

  Mgawo mwingine wa mapato hayo ni asilimia 15 ya uwanja sh. 15,287,156.92, tiketi sh. 3,145,790, gharama za mechi sh. 9,172,294.15, Kamati ya Ligi sh. 9,172,294.15, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 4,586,147.08 na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 3,567,003.28.
  Simba SC ilipunguzwa kasi jana na Mbeya City baada ya kulazimishwa sare ya 2-2 katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara Uwanja wa Taiafa, Dar es Salaam. 
  Pamoja na matokeo hayo, Simba SC bado inaongoza Ligi Kuu kwa kufikisha pointi 11 baada ya kucheza mechi tano, wakati Mbeya City inafikisha pointi saba baada ya mechi tano pia. 
  Katika mchezo huo uliochezeshwa na refa Abdallah Kambuzi wa Shinyanga, Charles Mbilinyi na Juma Mwita wa Mwanza, hadi mapumziko, tayari Simba SC walikuwa mbele kwa mabao 2-1.
  Simba SC inayofundishwa na mshambuliaji wake wa zamani, Abdallah Athumani Seif ‘King Kibaden’, ilipata mabao yake yote kupitia kwa Amisi Tambwe aliyefunga katika dakika za 29 na 33.
  Mbeya City, timu ya Halmashauri ya Jiji la Mbeya inayofundishwa na Juma Mwambusi, bao la la kipindi cha kwanza lilifungwa na Paul Nonga dakika ya 37, wakati la kusawazisha lilifungwa na Richard Peter dakika ya 69.
  Tambwe alifunga bao lake la kwanza akiunganisha krosi ya Chanongo, wakati la pili ilikuwa pasi ya Betram Mombeki.
  Paul Nonga alifunga bao lake kwa shuti kali ambalo lilimshinda kpa wa Simba SC, Abbel Dhaira Peter alifunga bao lake akiunganisha mpira wa adhabu uliopigwa na Mwagane Peter.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments
  Item Reviewed: SIMBA, MBEYA CITY ZAINGIZA MILIONI 123 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top