• HABARI MPYA

    Wednesday, September 18, 2013

    REAL MADRID YAWAFUMUA AKINA DROGBA WIKI NZIMA NYUMBANI KWAO...BALE ANG'ARA, RONALDO ATISHA MBAYA

    IMEWEKWA SEPTEMBA 18, 2013 SAA 7:07 USIKU
    NYOTA Gareth Bale ametokea benchi na kupikia mabao mawili Real Madrid ikiitandika Galatasaray mjini Istanbul mabao 6-1 huku Cristiano Ronaldo akipiga hat-trick yake ya 21 Bernabeu.
    Bale aliwashuhudia Isco, Karim Benzema na Ronaldo wakiiweka klabu yake mbele kwa mabao 3-0 kabla ya kuingia na kutoa mchango wake kunenepesha ushindi. 
    Kwanza, ilikuwa mpira wa adhabu wa winga huyo wa Wales uliomkuta Ronaldo, ambaye akaifungia bao la nne timu ya Carlo Ancelotti. Kisha akampa pasi Ronaldo, ambaye alimpasia pia Benzema kabla ya mshambuliaji huyo wa Ufaransa kufunga bao lake la pili katika mchezo huo. 
    Isco alifunga dakika ya 33, Benzema 54 na 81 Ronaldo 63, 66 na 90, wakati bao la kufutia machozi la wenyeji lilifungwa na Bulut dakika ya 84.
    Didier Drogba alicheza kwa dakika 45 tu kabla ya kutolewa na nafasi yake kuchukuliwa na Amrabat. 
    Kikosi cha Real Madrid kilikuwa: Casillas/Lopez dk14, Carvajal, Ramos, Pepe, Arbeloa, Modric/Illarramendi dk72, Khedira, Di Maria, Isco/Bale dk64, Ronaldo na Benzema
    Galatasaray: Muslera, Eboue, Chedjou, Nounkeu, Riera, Inan, Melo, Baytar/Bruma dk62, Yilmaz, Sneijder na Drogba/Amrabat dk46.
    Match ball's mine: Cristiano Ronaldo put the ball inside his shirt after netting a hat-trick in Istanbul
    Anaondoka na mpira wake: Cristiano Ronaldo akiwa ameweka mpira kwenye jezi yake baada ya kufunga Hat-trick mjini Istanbul

    Katika mechi nyingine, Man Utd imeshinda  4 -2 dhidi ya Bayer Leverkusen, Real Sociedad imefungwa nyumbani 2-0 na Shakhtar Donetsk, FC Copenhagen imetoa  1 - 1 na Juventus, Benfica imeifunga 2 - 0  Anderlecht, Olympiacos imefungwa 4-1 nyumbani na  PSG, Bayern Munich imeichapa 3 - 0 CSKA Moscow wakati Plzen imefungwa 3-0 nyumbani na Man City.


    MATOKEO KAMILI NA WAFUNGAJI LIGI YA MABINGWA:

    17 September
    Man Utd4 - 2Bayer Leverkusen
    Wayne Rooney (21)
    Robin van Persie (58)
    Wayne Rooney (69)
    Antonio Valencia (78)
    Simon Rolfes (53)
    Omer Toprak (87)
    Old Trafford
    Report
    17 September
    Real Sociedad0 - 2Shakhtar Donetsk
    Santos Alex Teixeira (64)
    Santos Alex Teixeira (86)
    Anoeta
    Report
    17 September
    FC Copenhagen1 - 1Juventus
    Nicolai Jorgensen (13)Fabio Quagliarella (53)
    Parken
    Report
    17 September
    Galatasaray1 - 6Real Madrid
    Umut Bulut (83)Alarcon Isco (32)
    Karim Benzema (53)
    Cristiano Ronaldo (62)
    Cristiano Ronaldo (65)
    Karim Benzema (80)
    Cristiano Ronaldo (90)
    Turk Telekom Arena
    Report
    17 September
    Olympiacos1 - 4PSG
    Vladimir Weiss (24)Edinson Cavani (19)
    Santos Thiago Motta (67)
    Santos Thiago Motta (72)
    Aoas Correa Marquinhos (85)
    Karaiskakis Stadium
    Report
    17 September
    Benfica2 - 0Anderlecht
    Filip Djuricic (3)
    Anderson Luisao (29)
    Estadio da Luz
    Report
    17 September
    Bayern Munich3 - 0CSKA Moscow
    David Alaba (2)
    Mario Mandzukic (40)
    Arjen Robben (67)
    Allianz Arena
    Report
    17 September
    Plzen0 - 3Man City
    Edin Dzeko (47)
    Yaya Toure (52)
    Sergio Aguero (57)
    Struncovy Sady
    Report
    Nice work: Cristiano Ronaldo hugs Gareth Bale after his second goal of the evening
    Kazi nzuri: Cristiano Ronaldo akikumbatiana na Gareth Bale baada ya kufunga bao lake la pili
    World's most expensive... sub: Bale came off the bench to help Real Madrid cruise past Galatasaray
    Mchezaji ghali duniani...anatokea benchi: Bale aliingia kipindi cha pili kuisaidia Real Madrid kuisambaratisha Galatasaray
    Expensive duo: Gareth Bale (right) walks alongside Cristiano Ronaldo as he celebrates his second goal
    Wawili ghali: Gareth Bale (kulia) akiongozana na Cristiano Ronaldo wakati akishangilia bao lake la piliFlying high: Cristiano Ronaldo celebrates his first goal for Real Madrid
    ameenda hewani: Cristiano Ronaldo akishangilia bao lake la kwanza
    Nice work: Karim Benzema celebrates Real's second goal
    Kazi nzuri: Karim Benzema akishangilia bao lake
    Silenced: Isco popped up to open the scoring for Real Madrid, despite the din coming from Galatasaray's fans
    Kimya kimya: Isco alifunga bao la kwanza
    Frustration: Cristiano Ronaldo gestures towards the referee after being brought down
    Hasira: Cristiano Ronaldo akimlalamikia refa baada ya kuangushwa
    Benched: Gareth Bale watched the first half of the match from the sidelines
    Benchi: Gareth Bale akiangalia mechi kutokea benchi kipindi cha kwanza kabla ya kuingia na kufanya kazi nzuri
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: REAL MADRID YAWAFUMUA AKINA DROGBA WIKI NZIMA NYUMBANI KWAO...BALE ANG'ARA, RONALDO ATISHA MBAYA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top