• HABARI MPYA

    Saturday, September 21, 2013

    MBEYA CITY WANYAMAZISHA SIMBA SC TAIFA

    Na Mahmoud Zubeiry, IMEWEKWA SEPTEMBA 21 2013 SAA 12:15 JIONI
    SIMBA SC imepunguzwa kasi leo na Mbeya City baada ya kulazimishwa sare ya 2-2 katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara Uwanja wa Taiafa, Dar es Salaam. 
    Pamoja na matokeo hayo, Simba SC bado inaongoza Ligi Kuu kwa kufikisha pointi 11 baada ya kucheza mechi tano, wakati Mbeya City inafikisha pointi saba baada ya mechi tano pia. 
    Katika mchezo huo uliochezeshwa na refa Abdallah Kambuzi wa Shinyanga, Charles Mbilinyi na Juma Mwita wa Mwanza, hadi mapumziko, tayari Simba SC walikuwa mbele kwa mabao 2-1.
    Mshambuliaji wa Simba SC, Amisi Tambwe akimtoka beki wa Mbeya City Anthony Matogolo katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara jioni ya leo. Timu hizo zilitoka 2-2.  

    Simba SC inayofundishwa na mshambuliaji wake wa zamani, Abdallah Athumani Seif ‘King Kibaden’, ilipata mabao yake yote kupitia kwa Amisi Tambwe aliyefunga katika dakika za 29 na 33.
    Mbeya City, timu ya Halmashauri ya Jiji la Mbeya inayofundishwa na Juma Mwambusi, bao la la kipindi cha kwanza lilifungwa na Paul Nonga dakika ya 37, wakati la kusawazisha lilifungwa na Richard Peter dakika ya 69.
    Tambwe alifunga bao lake la kwanza akiunganisha krosi ya Chanongo, wakati la pili ilikuwa pasi ya Betram Mombeki.
    Paul Nonga alifunga bao lake kwa shuti kali ambalo lilimshinda kpa wa Simba SC, Abbel Dhaira Peter alifunga bao lake akiunganisha mpira wa adhabu uliopigwa na Mwagane Peter.
    Mabao sita, mechi tano; Amisi Tambwe amefunga mabao mawili leo

    Kikosi cha Simba SC kilikuwa; Abbel Dhaira, William Lucian ‘Gallas’, Issa Rashid ‘Baba Ubaya’, Kaze Gilbert/Hassan Hatibu dk66, Joseph Owino, Jonas Mkude, Twaha Ibrahim/Ramadhani Chombo ‘Redondo’ dk50, Amri Kiemba/Ramadhani Singano ‘Messi’ dk79, Betram Mombeki, Amisi Tambwe na Haroun Chanongo. 
    Mbeya City; David Burhan, John Kabanda, Hassan Mwasapili, Deogratius Julius, Antony Matogolo, Yohana Morris, Mwagane Yeya/Richard Peter dk59, Steven Mazanda, Paul Nonga, Deus Kaseke na Yussuf Willson.   
    Katika mechi nyingine, Uwanja wa Mkwakwani, Tanga wenyeji Mgambo Shooting Stars walitoka sare ya 1-1 na Rhino Rangers ya Tabora, Prisons ilitoka 1-1 na Mtibwa Sugar Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine mjini Mbeya, wakati Kagera Sugar ilishinda 3-0 dhidi ya Ashanti United ya Dar es Salaam Uwanja wa Kaitaba.
    Ligi hiyo itakamilisha mzunguko wake wa tano kesho kwa mechi tatu moja ndiyo hiyo ya Azam na Yanga Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam huku JKT Ruvu ikikwaruzana na Oljoro JKT kwenye Uwanja wa Azam Complex.
    Ruvu Shooting inayokamata nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi itakuwa mgeni wa Coastal Union katika mechi itakayopigwa kwenye Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: MBEYA CITY WANYAMAZISHA SIMBA SC TAIFA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top