• HABARI MPYA

  Jumanne, Septemba 17, 2013

  KIPUTE AIRTEL RISING STARS CHAANZA AGEGE

  Na Prince Akbar, IMEWEKWA SEPTEMBA 17, 2013 SAA 6:48 MCHANA 
  TIMU zinazoshiriki michauano ya pili ya Afrika ya Airtel rising Stars inayofanyika nchini Nigeria mwaka huu zimewasili ambapo michuano hiyo imeanza rasmi jana katika viwajnja vya Agege, Lagos huku nyota wa zamani wa soka dunani, akiwemo Mfaransa Robert Pires aliyewika Arsenal ya England wakihudhuria.
  Timu ya Zambia ilikuwa ya kwanza kutua siku ya Ijumaa ikifuatiwa na Ghana iliyotua muda mchache baadaye siku hiyo. Mabingwa watetezi, Niger walitua katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Murtala Mohammed Jumamosi  mchana pamoja na Kongo Brazzaville.
  Timu ya Tanzania ikitambulishwa

  Kikosi cha  Tanzania kiliwasili Jumapaili chini ya kocha, Abel Mtweve na timu nyingine zilitarajiwa kuwasili kabla ya michuano hiyo kuanza jana.
  Airtel Rising Stars ni michuano ya kipekee ya nchi za Afrika yenye lengo la kuvumbua na kukuza vipaji  huku ikiwezesha nchi za Afrika kupata wachezaji wa timu za taifa kwa kupitia mashindano haya Airtel inatoa nafasi kwa vijana hawa kutimiza ndoto zao, na kuonyesha uwezo wao kwa zaidi ya mamilioni ya watu alisema mkurugenzi mkuu wa Airtel Nigeria, Segun Ogunsanya.
  “Wachezaji wengi wameshiriki michuano mikubwa kama hii kwa mara ya kwanza na wanafurahia kupata nafasi ya kushindana na wachezaji nyota wengine toka katika nchi mbalimbali. kwa wiki nzima tunaamini wachezaji hawa watabaki na kumbukumbu ya mpira ambayo wataifurahia katika maisha yao siku zote,”alisema.
  Michuano ya Airtel Rising Stars ilianza jana mjini Lagos, Nigeria hadi Septemba 22 mwaka huu. Wachezaji nyota waliochaguliwa watashiriki katika kliniki  itakayosimamiwa na makocha wa Manchester United inayotegemewa kufanyiaka Aprili mwakani mjini Lubumbashi, DRC.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments
  Item Reviewed: KIPUTE AIRTEL RISING STARS CHAANZA AGEGE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top