• HABARI MPYA

    Tuesday, September 03, 2013

    SIRI NYINGINE IMEFICHUKA OLD TRAFFORD, UNITED ILIJARIBU TENA KUMSAJILI SNEIJDER KUTOKA GALATASARAY IKADUNDA

    IMEWEKWA SEPTEMBA 3, 2013 SAA 4:30 USIKU
    KLABU ya Galatsaray ya Uturuki imesema Manchester United ilitoa ofa ya kumnunua kiungo wake mwenye umri wa miaka 29, Wesley Sneijder. 
    United awali ilikaribia kumsajili kiungo huyo Mholanzi kutoka Inter Milan mwaka 2011 kwa dau la Pauni Milioni 35, lakini iliamua kuachana na Sneijder baada ya kutaka mshahara wa Pauni 200,000 kwa wiki. 
    Pamoja na hayo, sasa inasemekana United ilifufua mpango wa kumsajili mchezaji huyo chini ya kocha wake mpya, David Moyes, huku Galatasaray ikisema klabu hiyo ya Old Trafford ilimgeukia Sneijder baada ya kukwama kuwasajili Cesc Fabregas na Thiago Alcanatara mapema majira haya ya joto. 
    Staying put: Wesley Sneijder in training with the Holland squad in Katwijk on Tuesday
    Wamemkosa tena: Wesley Sneijder akiwa mazoezini na Uholanzi nchini Katwijk leo
    Staying put: Wesley Sneijder in training with the Holland squad in Katwijk on Tuesday
    Anabaki: Wesley Sneijder yuko mazoezini  na kikosi cha Uholanzi nchini Katwijk leo
    Dutch of class: Holland boss Louis van Gaal addresses his squad ahead of this week's World Cup qualifiers
    Mholanzi kiwango: Kocha wa Uholanzi, Louis van Gaal anakiandaa kikosi chake kwa mechi ya kufuzu Kombe la Dunia wiki hii

    Mratibu wa Michezom, Bulunt Tulun ameliambia gazeti la Uturuki, Milliyet kwamba: "Sneijder amepokea ofa kutoka Manchester United wiki mbili zilizopita, lakini haikukubaliwa. Kulikuwa kuna klabu kadhaa zinamtaka, lakini kama ambavyo hatuwezi kumruhusu kuondoka Burak (Yilmaz) pia tunatakiwa kumbakiza Sneijder,"alisema.
    Roma ilithibitisha United ilitoa ofa ya wazi kwa ajili ya Daniele De Rossi ya Pauni Milioni 12, ambayo ilipigwa chini pia, wakati Mktendaji Mkuu, Ed Woodward aliripotiwa kujaribu kumsajili kwa Pauni Milioni 30.5 kiungo wa Athletic Bilbao, Ander Herrera. 
    Rejected: United missed out on Sami Khedira (top), Daniele De Rossi (below) and Ander Herrera (bottom)
    Imedunda: United imemkosa pia Sami Khedira (juu), Daniele De Rossi (chini) na Ander Herrera (chini kabisa)
    Rejected: United missed out on Sami Khedira (top), Daniele De Rossi (below) and Ander Herrera (bottom)
    Rejected: United missed out on Sami Khedira (top), Daniele De Rossi (below) and Ander Herrera (bottom)
    United pia ilikwama kumsajili mwanasoka wa kimataifa wa Ujerumani, Sami Khedira ahamie Old Trafford kutoka Real Madrid, na kiungo huyo amethibitisha mwenyewe alivyokoswakoswa na kocha David Moyes dakika za mwishoni. 
    United imefanikiwa tu kumsajili kiungo Mbelgiji wa Everton, Marouane Fellaini kwa Pauni Milioni 27.5, anayekwenda kuungana na kocha wake wa zamani Toffees, David Moyes Old Trafford.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: SIRI NYINGINE IMEFICHUKA OLD TRAFFORD, UNITED ILIJARIBU TENA KUMSAJILI SNEIJDER KUTOKA GALATASARAY IKADUNDA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top