• HABARI MPYA

  Jumapili, Juni 30, 2013

  THIAGO SASA HUENDA AKAOTA MBAWA MAN UNITED, ASEMA; "NAIPENDA BARCELONA"

  IMEWEKWA JUNI 30, 2013 SAA 4:16 USIKU
  KLABU ya Barcelona ilifanya mazungumzo na mchezaji anayetakiwa na Manchester United, Thiago Alcantara wiki iliyopita katika jitihada za kumzuia asitimkie Old Trafford na kutoka na alichoandika hivi sasa katika ukurasa wake wa - Tweeter kuna wasiwasi.
  Akiwa ametulia kwenye bwawa la kuogelea na kaka yake, Rafinha ambaye ameongeza Mkataba wa kazi Nou Camp kwa miaka miwili zaidi hadi mwaka 2016 mapema wiki hii, Thiago alitweet: "Naipenda Barcelona,".
  Mabingwa hao wa Ligi Kuu England waliaminika kufikia makubaliano juu ya maslahi binafsi, ikiwemo mshahara wa Pauni Milioni 5.5 kwa mwaka na mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22 na wakatumai kumnunua kwa Pauni Milioni 17.
  Affection: Thiago Alcantara (left) posted this snap with brother Rafinha and the caption 'I love Barcelona'
  Utata: Thiago Alcantara (kushoto) ameposti picha akiwa na Rafinha na maelezo chini;  "Naipenda Barcelona"
  Champion: Thiago shot to worldwide recognition by scoring a hat-trick in the Euro U21 final against Italy
  Bingwa: Thiago aliiwezesha Hispania kutwaa Kombe la Euro kwa vijana chini ya umri wa miaka 21, akifunga mabao matatu peke yake dhidi ya Italia katika fainali
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments
  Item Reviewed: THIAGO SASA HUENDA AKAOTA MBAWA MAN UNITED, ASEMA; "NAIPENDA BARCELONA" Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top