• HABARI MPYA

  Jumatano, Juni 26, 2013

  KONE AWAAMBIA WIGAN ANATAKA KUTUA EVERTON KWA BABA YAKE MARTINEZ

  IMEWEKWA JUNI 26, SAA 5:57 ASUBUHI
  MSHAMBULIAJI Arouna Kone anayetaka kuondoka amewaambia Wigan anataka kusaini Everton akiondoka Uwanja wa DW.
  Timu zote, Norwich na Swansea ziko tayari kulipa Pauni Milioni 6 kuununua Mkataba wa mchezaji huyo.
  Lakini nyota huyo wa Ivory Coast anataka kuungana na kocha wake wa zamani, Roberto Martinez, ambaye amehamia Goodison Park mwezi uliopita.
  Get me to Goodison: Arouna Kone wants to rejoin former manager Roberto Martinez at Everton
  Nipelekeni Goodison: Arouna Kone anataka kuungana na kocha wake wa zamani, Roberto Martinez klabu ya Everton
  New job: Roberto Martinez took over as Everton boss this summer as he replaced David Moyes
  Kazi mpya: Roberto Martinez amekuwa kocha wa Everton kuchukua nafasi ya David Moyes

  Alikuwa Martinez aliyemvuta Kone, mwenye umri wa miaka 29, England miezi 12 iliyopita kwa Pauni Milioni 3.5 kutoka Levante.
  Na mshambuliaji huyo anaamini Mspanyola huyo anaweza kumfanya aendelee kuwa bora katika Ligi Kuu ya England.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments
  Item Reviewed: KONE AWAAMBIA WIGAN ANATAKA KUTUA EVERTON KWA BABA YAKE MARTINEZ Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top