• HABARI MPYA

  Alhamisi, Juni 20, 2013

  MESSI NA BABA YAKE KUPANDISHWA KIZIMBANI KWA KUKWEPA KODI HISPANIA...WAKIKUTWA NA HATIA JELA MIAKA SITA

  IMEWEKWA JUNI 20, 2013 SAA 3:20 USIKU
  MSHAMBULIAJI wa Barcelona, Lionel Messi na baba yake, Jorge watapanda kizimbani katika Mahakama ya Hispania Septemba katika sehemu ya kujibu tuhuma zao za kukwepa kodi.
  Wawili hao wametakiwa kuhudhuria Mahakamani Gava, Catalonia, Jumanne ya September 17 kujibu maswali ya kukwepa kodi Hispania kiasi chaEuro Milioni 4 (Pauni Milioni3.4) kati ya mwaka 2007 na 2009.
  Taarifa kutoka kwa Waziri wa Sheria imesema: "Korti namba 3 ya Gava imekubali imekubali kufungua mjadala uliowasilishwa na mwendesha mashitaka dhidi ya Lionel Andres Messi na Jorge Horacio Messi kwa mashitaka matatu dhidi ya Wizara ya Fedha, kuhusiana na ukwepaji kodi kwa miaka ya  2007, 2008 na 2009 na akikutwa na hatia atafungwa jela miaka sita.
  Summoned: Lionel Messi and his father Jorge Horacio have been summoned for questioning by a Spanish court over tax fraud allegations
  Kizimbani: Lionel Messi na baba yake, Jorge Horacio wanakabiliwa mashitaka ya ukwepaji kodi Hispania

  Nyota huyo wa Argentina, Messi, mwenye umri wa miaka 25, wiki iliyopita aliandika katika ukurasa wake wa Facebook akikanusha kuhusu yeye au baba yake kuhusika uovu wowote.
  Taarifa ya Mwanasoka huyo bora wa Dunia wa FIFA imesema: "Tunafahamu kupitia vyombo vya habari kuhusu madai yaliyofunguliwa na Mamlaka ya Mapato ya Hispania.
  Father and son: Messi posing with his dad Jorge Horacio Messi (R) in 2008
  Baba na mwana: Messi akiwa na baba yake Jorge Horacio Messi (kulia) mwaka 2008
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments
  Item Reviewed: MESSI NA BABA YAKE KUPANDISHWA KIZIMBANI KWA KUKWEPA KODI HISPANIA...WAKIKUTWA NA HATIA JELA MIAKA SITA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top