• HABARI MPYA

  Jumanne, Juni 18, 2013

  HISPANIA WAIFUMUA 4-2 ITALIA NA KUTWAA UBINGWA WA ULAYA U21

  Champions: The Spanish U21 stars are jubiliant as they celebrate by lifting the trophy after their 4-2 win
  Mabingwa: Nyota wa U21 ya Hispania wakishangilia na taji lao baada ya kuifumua Italia 4-2
  Spain
  IMEWEKWA JUNI 18, 2013 SAA 3:30 USIKU
  KIUNGO Thiago Alcantara amekuwa kivutio katika ushindi wa kikosi cha vijana cha Hispania chini ya miaka 21 wa mabao 4-2 dhidi ya Italia na kutwaa Kombe la Ulaya kwa vijana barani humo, baada ya mchezaji huyo anayetakiwa na Manchester United kufunga mabao matatu mjini Jerusalem.
  Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22 wa Barcelona amekuwa akihusishwa kwa kiasi kikubwa na kuhamia Old Trafford.
  Alcantara, aliyekuwamo kwenye kikosi cha Hispania kilichoshinda taji hilo miaka miwili iliyopita nchini Denmark, aliifungia timu yake bao la kwanza dakika ya sita, lakini Italia ikasawazisha haraka kupitia kwa Ciro Immobile dakika ya 10.
  Thiago akafunga tena dakika ya 31 na 38 kwa penalti, kabla ya Isco kufunga dakika ya 66 kwa penalti pia na Borini akaifungia Italia dakika ya 79 kufanya 4-2.
  Kikosi cha Hispania leo kilikuwa; De Gea, Montoya, Bartra, Martinez, Moreno, Koke/Camacho dk86, Illarramendi, Thiago, Tello/Muniain dk70, Morata/Rodrigo dk80 na Isco.
  Italy U21; Bardi, Donati, Bianchetti, Caldirola, Regini, Florenzi/Saponara dk58, Rossi, Verratti/Crimi dk76, Insigne, Borini na Immobile/Gabbiadini dk58.Hat-trick hero: Thiago Alcantara netted three goals in the first half to set Spain on their way
  Shujaa wa Hat-trick: Thiago Alcantara amefunga mabao matatu kipindi cha kwanza kuipa ushindi Hispania
  Group hug: Spain's youngsters celebrate Isco's goal, putting them 4-1 up
  Nyota wa Hispania wakishangilia bao la Isco
  Despair: Alessandro Florenzi of Italy can't bear to watch as Spain run riot
  Alessandro Florenzi wa Italia
  Effort: Italy's forward Lorenzo Insigne (left) advances with the ball past Spain's defender Martin Montoya
  Lorenzo Insigne wa Italia (kushoto) akimtoka beki wa Hispania, Martin Montoya
  Battle: Aberto Moreno of Spain tries to tackle Ciro Immobile of Italy as the Italian advances past
  Aberto Moreno wa Hispania akijaribu kumpitia Ciro Immobile wa Italia
  Hero: Thiago Alcantara (centre) celebrates his third goal with Cristian Tello (front) and Alvaro Morata
  Shujaa: Thiago Alcantara (katikati) akishangilia bao lake la tatu na Cristian Tello (mbele) na Alvaro Morata
  Dispute: Giulio Donati, Matteo Bianchetti and Marco Verratti (L-R) appeal against a penalty decision
  Kutoka kushoto; Giulio Donati, Matteo Bianchetti na Marco Verratti wakilalamikia penalti
  Tussle: Spain forward Cristian Tello (left) challenges Italy's Lorenzo Insigne for the ball
  Cristian Tello wa Hispania (kushoto) akikabiliana na Lorenzo Insigne wa Italia
  Flying tackle: Spain's Montoya (left) goes straight into a tackle with Vasco Regini of Italy
  Montoya wa Hispania (kushoto) akienda chini baada ya kupitiwa na Vasco Regini wa Italia
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments
  Item Reviewed: HISPANIA WAIFUMUA 4-2 ITALIA NA KUTWAA UBINGWA WA ULAYA U21 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top