• HABARI MPYA

  Jumamosi, Juni 29, 2013

  MKENYA WANYAMA NI KAMA TAYARI YUPO LIGI KUU ENGLAND, KLABU GANI? HILO NDILO SUALA

  IMEWEKWA JUNI 29, 2013 SAA 7:59 MCHANA
  KLABU ya Cardiff City imejitoa kwenye mbio za kuwania saini ya Victor Wanyama baada ya klabu yake, Celtic kushindwa kuidhinisha ofa waliyotoa kwa ajili ya kiungo huyo.
  Kocha wa Cardiff, Malky Mackay bado anamtaka sana Mkenya huyo na amepandisha ofa yake baada ya ile awali ya Pauni Milioni 10 kukataliwa na Peter Lawwell Jumatatu.
  Celtic tayari imekubali Pauni Milioni 12 kutoka Southampton wiki iliyopita, lakini mawakala wa kiungo huyo, Rob Moore na Ivan Modia, wamekataa kutokana na kutoridhishwa na vipengele vya maslahi binafsi ya mchezaji.
  Wanted man: Celtic midfielder Victor Wanyama (centre) is the subject of an improved bid from Cardiff
  Mtu anayetakiwa: Kiungo wa Celtic, Victor Wanyama (katikati) anayetakiwa na Cardiff

  BIN ZUBEIRY inafahamu Cardiff imekwishafikia makubaliano na wawakilishi wa Wanyama juu ya mshahara anaotaka mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22.
  Sasa klabu hiyo ya Parkhead lazima iamue aidha kutoa fursa ya mazungumzo rasmi kuanza — na Cardiff inajiandaa kupanda dau.
  Kocha wa Celtic, Neil Lennon anaamini kiungo huyo amekwishacheza mechi yake ya mwisho katika klabu hiyo, na anaamini mchezaji huyo ataondoka wakati wowote.
  Remember the name: Wanyama looks certain to leave Celtic this summer for the Premier League in England
  Kumbuka jina hilo: Wanyama anaonekana anataka kuhamia Celtic akacheze Ligi Kuu ya England
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments
  Item Reviewed: MKENYA WANYAMA NI KAMA TAYARI YUPO LIGI KUU ENGLAND, KLABU GANI? HILO NDILO SUALA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top