• HABARI MPYA

    Tuesday, June 18, 2013

    LIVERPOOL YAKUBALI 'POTELEA MBALI' SUAREZ, WAMTAKA AWASILISHE BARUA RASMI YA KUOMBA KUONDOKA

    IMEWEKWA JUNI 18, 2013 SAA 1:50 ASUBUHI
    KLABU ya Liverpool itamtaka Luis Suarez aandike barua rasmi juu ya nia yake ya kuondoka katika klabu hiyo ili kuamua mustakabali wake.
    Mwanasoka huyo wa kimataifa wa Uruguay, ambaye kwa sasa anacheza Kombe la Mabara, amezungumza mara kadhaa kwenye vyombo vya habari juu ya mpango wake kutaka kuondoka Anfield majira haya ya joto, lakini, bado hajaupa taarifa rasmi uongozi wa Liverpool.
    Ikiwa Suarez atauzwa kwa Real Madrid, kama anavyotaka, Liverpool itakubali akiwasilisha barua rasmi ya maombi, wakati pia watataka ada ya uhamisho ya Pauni Milioni 50. Hadi sasa, Madrid haijawasilisha maombi rasmi ya kutaka kumnunua mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26.
    International duty: Luis Suarez has been representing Uruguay
    Majukumu ya kimataifa: Luis Suarez anawaikilisha Uruguay

    Liverpool bado inafanya mipango ya msimu ujao pamoja na kwamba haijui kama Suarez atabakia, lakini uhalisia ni kwam ba wanajua itakuwa vigumu kumbakiza baada ya matukio yote dhidi yake katika miezi iliyopita.
    Ni kwa sababu hizo klabu inataka suala hilo litatuliwe haraka iwezekanavyo.
    Kocha Brendan Rodgers, ambaye hadi sasa amemsajili Kolo Toure pekee, anataka kuongeza mabao katika timu yake na Liverpool inataraji kupata uhamisho wa kimataifa saa 24 zijazo kukamilisha uhamisho wa mshambuliaji wa Celta Vigo, Iago Aspas.
    Iago Aspas
    Simon Mignolet
    Wanaongezwa? Simon Mignolet anatarajiwa kuungana na Iago Aspas Anfield

    Aspas anatarajiwa kufuatiwa na winga wa Sevilla, Luis Alberto, wakati mazungumzo yamefikia hatua nzuri kukamilisha usajili wa kipa wa Sunderland, Simon Mignolet. Uhamisho wake ambao unatarajiwa kugharimu Pauni Milioni 10, unaweza kueleweka hadi mwishoni mwa wiki.
    Mustakabali wa Andy Carroll baada ya kuomba kuondoka, unatarajiwa kujulikana kabla ya mwishoni mwa wiki.Mshambuliaji huyo wa England, ambaye yupo mapumziko nje, amekubali alifikia makubaliano binafsi na West Ham mwezi uliopita na Liverpool wanataka kumuuza mchezaji huyo kwa Pauni Milioni 15. Kitu kinachotakiwa kwake hivi sasa ni kufaulu vipimo vya afya.
    Departing: Andy Carroll is nearing a permanent transfer to West Ham
    Anaondoka: Andy Carroll anakaribia kuhamishiwa moja kwa moja West Ham
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: LIVERPOOL YAKUBALI 'POTELEA MBALI' SUAREZ, WAMTAKA AWASILISHE BARUA RASMI YA KUOMBA KUONDOKA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top