• HABARI MPYA

  Ijumaa, Juni 28, 2013

  JANJA YA BARCELONA KUMLAINISHA THIAGO ASIENDE MAN UNITED, WAMUONGEZEA MKATABA MDOGO WAKE RAFINHA

  IMEWEKWA JUNI 28, 2013 SAA 8:39 MCHANA
  KLABU ya Barcelona imekubali kusaini Mkataba mpya na Rafael 'Rafinha' Alcantara ili kuendelea kuishi na mdogo huyo wa Thiago hadi mwaka mwaka 2016.
  Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 20, sasa anaweza kutumika kama ushawishi kwa kaka yake, Thiago na klabu hiyo Katalunya ili asikubali kuhamia Manchester United anakotakiwa abaki.
  Awali, Rafinha alihusishwa na kuhamia Ligi Kuu England ambako kaka yake, Thiago pia yuko njiani kuhamia.
  New deal: Rafinha Alcantara has signed a contract extension at Barcelona
  Mkataba mpya: Rafinha Alcantara amesaini Mkataba wa kuendeela kukipiga Barcelona
  Transfer blow: The news will come as a blow to Manchester United who were hoping a Rafinha move to England would increase their chances of landing older brother Thiago
  Pigo: Habari hizi zinaweza kuwa pigo kwa Manchester United ambayo ilitarajia Rafinha kuhamia England angesaidia wao kumpata kaka yake, Thiago
  Lakini klabu hiyo ya Catalan inatarajiwa kuwa na mazungumzo na kiungo huyo anayetaka kuondoka, ambaye amekubali mshahara wa Pauni Milioni 5.5 kwa mwaka kutoka United baada ya kushindwa kupata uhakika wa namba katika kikosi cha kwanza msimu uliopita.
  Mkataba wake unasema anatakiwa acheze kwa asilimia 60 kikosi cha kwanza, kitu ambacho hakikufikiwa.
  Barcelona inataka mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22 abaki na imemuhakikishia atakuwa kiongozi wa timu baada ya Xavi na Iniesta kueonekana wanalekea 'uzeeni'.
  Rafinha, ambaye ameamua kufuata uraia wa baba yake, Mazinho Brazil, badala ya Hispania kwa mama, alitwaa Kombe la Dunia na Brazil na ameichezea mechi 36 Barcelona B msimu uliopita, akifunga mabao 10 kikosi hicho cha wachezaji wa akiba kikishika nafasi ya nane Ligi ya Segunda. 
  Switching allegiance: Rafinha switched from playing for Spain to play for Brazil
  Kubadili uraia: Rafinha amebadili uraia kutoka Hispania hadi Brazil
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments
  Item Reviewed: JANJA YA BARCELONA KUMLAINISHA THIAGO ASIENDE MAN UNITED, WAMUONGEZEA MKATABA MDOGO WAKE RAFINHA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top